Wednesday, 10 September 2014

KAZI KWAKO HAPO:::Mzigo mpya wa iPhone6 umeuona? na saa iliyokuja nayo je? viko hapa

news news
Najua kuna uwezekano ukawa ulisikia fununu sana kuhusu iPhone6 au hata kuona baadhi ya taarifa feki kuhusu simu hii mpya, post hii ni maalum kukuletea taarifa sahihi na ya ukweli kuhusu iPhone6 ambayo ndio imetambulishwa rasmi.
Wanasema simu zote hizi mbili mpya zina A8 processor ambayo inafanya ziwe na kasi zaidi kuliko iPhone5 kwa asilimia 20.
iphone 6 1
Unaambiwa zote iPhone6 na iPhone6 plus zimekuja na screen kubwa tofauti na nyingine zilizotangulia
iphone 6 2
Apple wenyewe wanasema simu hizi mbili za iPhone6 na iPhone 6 plus zina 8 megapixel camera ambayo itasaidia camera kupata focus faster.
iphone 6 3
Simu hizi zote mbili zitaanza kupatikana nchini Marekani September 19 2014 nchini Marekani pamoja na kwenye nchi nyingine nane duniani.
iphone 6 4
Simu hizi za iPhone 6 na iPhone 6 pluz zitaambatana na saa hii ambayo unaweza kuitumia kufanya mambo mbalimbali ambayo yapo kwenye simu pia
iphone 6 5
Apple wanasema malengo yao ni k’uireplace’ au kuichukua nafasi ya Wallet, yani kurahisisha mambo kwenye iPhone kiasi kwamba hutohitaji kutembea na wallet.
Mengine yaliyosemwa ni pamoja na >>  ‘the bigger displays allow for bigger batteries: 11 hours of video watching on the iPhone 6 and 14 hours for the iPhone 6 Plus — up from 10 hours on the iPhone 5S‘
And the iPhones will come with Apple’s new iOS 8 software, featuring a new HealthKit application that monitors users’ heart rates, sleep, weight and blood pressure among other health-related information. Apple said iOS 8 will be available Sept. 17 to customers who have an iPhone 4S, iPhone 5, iPhone 5C or iPhone 5S.
iphone 6
<br /> >
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

ALIKIBA AKASOME KWA MWENDO HUU WA DIAMOND PLATNUMZZZ


Diamond apiga mbili kwa mpigo, ashinda tuzo Australia na atajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Neema inazidi kumuangia Diamond Platinumz na leo amepata habari njema baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV EMAs huku akipokea tuzo kutoka nchini Australia.
Diamond amewapa mashabiki wake habari njema za ushindi wa tuzo ya AAMA ya Australia kupitia tiketi ya collabo ya aliyopewa na Desert Eagle, wimbo unaoitwa ‘Everyday’.
“Ningependa niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the Year..).” Ameandika.
Wakati huo huo, mtoto wa Tandale ametajwa kuwa moja kati ya wasanii wanaowania MTV Europe Music Awards mwaka huu huku akichuana na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Davido, Toofan (Togo) na Goldfish (Afrika Kusini).
Msanii mwingine wa tano akisubiria kutajwa baada ya mashabiki kumpekeza kutoka kwenye kundi la wasanii sita ambao ni Anselmo Ralph, Gangs of Ballet, Mafikizolo, Sarkodie, Sauti Sol na Tiwa Savage.  
Aidha, majina yote ya wasanii wanaowania tuzo hizo yatatajwa September 16 ambapo upigaji kura utaanza rasmi.
Hongera Diamond Platinumz, Tanzania inazidi kutajwa kwenye majukwaa ya kimataifa.

MAMBO YA UMBEA TENA::NDOA YA LUCY KOMBA MIKOSI 3

Stori: Gladness Mallya na Mayasa Mariwata
ILE ndoa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya nyota wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba na mzungu wake raia wa Denmark anayejulikana kwa jina moja la Janus hatimaye imefungwa na kutawaliwa na matukio yenye mikosi kibao.
Nyota wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba na mzungu wake raia wa Denmark anayejulikana kwa jina moja la Janus wakiwa ni wenye furaha wakati wa harusi yao.
Ndoa hiyo ilifungwa Jumamosi iliyopita kwenye Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Mtakatifu Benedict lililopo maeneo ya Kurasini- Bandari jijini Dar.
Baada ya zoezi hilo kumalizika, wawili hao na wapambe wao walikwenda katika Kisiwa cha Bongoyo, Dar kwa ajili kupiga picha za ukumbusho. Kisiwa hicho kipo Kilomita 2.5 kutoka Pwani ya Jiji la Dar.
Mdenmark Janus akimwelekeza jambo mke wake rasmi Lucy Francis Komba.
Hata hivyo, zoezi la kwenda kupiga picha kwenye kisiwa hicho liliingia mkosi kufuatia maharusi hao kupanda  boti maeneo ya Slip Way, Oysterbay, Dar na kupigwa na mawimbi makubwa yaliyowafanya watumbukie baharini kabla ya kuokolewa na wapiga mbizi mahiri.
“Jamani sijui balaa gani hili? Yaani tumetumbukia baharini tukienda Bongoyo, viatu vimezama, nguo tulizovaa zimelowa,  tukaletewa nyingine, simu yangu pia iliingia majini lakini tunamshukuru Mungu tuliokolewa na kuendelea na safari,”alisema Lucy alipoulizwa na gazeti hili.
Wapambe wakijipanga kutoa sapoti katika harusi hiyo.
Lucy alisema walifika salama kisiwani Bongoyo na kupiga picha mbalimbali za ukumbusho na baada ya kumaliza walianza safari ya kurejea mjini ili kwenda kula na watoto yatima wa Kituo cha New Life kilichopo Kigogo jijini Dar lakini wakapata mkosi wa pili.
Lucy alisema hajui ni nini, kwani alishangaa sana baada ya kutoka Bongoyo wakiwa maeneo ya Kinondoni kuna gari lililoonekana kuwafuatilia toka mbali, liliwafikia na kuligonga gari lililokuwa katika msafara wake waliokuwa wakichukua matukio kwa kamera ya video, wakashuka na kuanza kuwafanyia fujo kisha wakawapora kamera hiyo na kuondoka kwa kasi eneo hilo.
Wanaharusi Lucy Komba na mumewe Janus wakipozi kupata picha ya ukumbusho.
“Sijajua mpaka sasa wale watu ni akina nani na walikuwa na dhamira gani, sijui walitumwa? Nashindwa kuelewa maana walikuwa mabaunsa wawili na mwanamke mmoja,” alisema Lucy.
Mbali na misukosuko yote waliyopata siku hiyo, lakini maharusi hao walifanikiwa kufika katika Ukumbi wa Makumbusho uliopo Posta Mpya, Dar ambapo sherehe ya kifahari ilifanyika na kuhudhuriwa na marafiki wa bi harusi na viongozi kutoka serikalini.
Mbali na yote, shughuli hiyo ilikuwa na vituko mbalimbali ambavyo viliwakosha waalikwa, ikiwemo watu wa kareti kutoa salamu zao za kikomandoo, mtu wa mazingaombwe ya nyoka, wanenguaji kutoka Kampuni ya Bia ya Windhoek kutoa shoo ya nguvu na msanii mkongwe Bongo, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’ kutumbuiza.
Maharusi wakiingia katika Ukumbi wa Makumbusho ulio Posta kwa ajili ya sherehe.
Bwana harusi naye alionesha mila ya kikwao kwa kulazwa chini na kuvuliwa viatu kisha kuvalishwa tena ikiwa ni ishara kwamba ameagana na ukapera.
Msanii huyo alipata zawadi kedekede kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake. Mama yake mzazi aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Marietta Minangi  alimzawadia kiwanja kilichopo Bunju jijini Dar huku baba yake mdogo (jina halikupatikana) akimpa mbuzi na ng’ombe wawili wa maziwa.Kaka yake alimkabidhi shilingi milioni tisa taslimu ukumbini hapo na kamati ya sherehe ilimpa shilingi milioni tatu bila kumsahau Dokii ambaye alimzawadia matofali 500 na mifuko 10 ya simenti.
Kutokana na thamani kubwa aliyonayo mzazi wake kwa kumzaa na kumlea vyema, Lucy alimfanyia ‘sapraizi’ mama yake huyo kwa kumpa zawadi ya gari aina ya Toyota Prado ambalo alimkabidhi mahali hapo.
“Namshukuru sana mama yangu kwa malezi mazuri aliyonipa mpaka sasa nimeolewa, sioni cha kumlipa kwa thamani kubwa aliyonayo kwangu, ila nimeamua kumzawadia gari aina ya Prado, japo ana gari lakini nimemzawadia hili ikiwa kama upendo wangu kwake,”alisema Lucy ambaye siku si nyingi anataraji kuondoka nchini kwenda Denmark kwa mumewe.

NYUMBA HIZI ZINAUZWA ZIPO IRINGA MJINI

 Nyumba  hii  ipo  eneo la Ilala  inauzwa  Tsh milioni 39
 Mwonekano  wake kwa  pembeni  pia  nyumba ina maji na umeme

 Umbali  wa  mita kama  7 ni barabara ya lami  ina hati  yake kamili
 Nyumba  hii  ipo  Ndiuka ina maji  inauzwa Tsh milioni 29
 ina huduma ya maji  imepigwa  lipu ndani umeme nguzo  ipo  nje  ila maeneo haya  bado hayajapimwa mkataba  upo
Mwonekano  wake wa nyuma
kutumba kwa mawasiliano na maelewano  zaidi  wasiliana nasi kwa namba  0754 026 299

Ripoti: Tanzania Yaongoza Kulalamikiwa kwa Matumizi Mabaya ya Instagram Duniani



Mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji picha umeendelea kupata mashabiki wengi nchini Tanzania lakini wengi kati ya watumiaji hao wameisababisha kuwa kati ya nchi zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya mtandao huo duniani kote.

Ripoti hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasialiano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy katika mahojiano maalum aliyofanya na Ibrahim Issa wa 100.5 Times Fm.

“Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeongoza kwa watu kulalamika kwamba matumizi yetu hayaendani na makusudio. Na hii inatokana na pale watu ambao wanawafuata watu wa` Tanzania kuona vitu wanavyoweka vitu wanavyoweka, ugomvi, matusi, picha za ajabu…za ngono na nini. Sasa watu huwa wanalalamika.” Amesema Innocent Mungy.

“Wanapolalamika, ule mtandao huwa unaweka record kwamba watu wengi waliolalamika kwenye mtandao huu kuhusu picha za watumiaji ambao wako Tanzania labda ni 20 wakilinganisha na sehemu nyingine ambazo idadi inakuwa ndogo zaidi.” Ameongeza.

Amefafanua kuwa kwenye mitandao yote ya kijamii, wakati wa kujiunga mtumiaji hupewa maelezo ya kurasa kadhaa kuhusu namna ya kutumia mtandao huo ikiwa ni pamoja na makatazo lakini watumiaji wengi wa Tanzania huwa hawayafuatilii/huyapuuza.

Mwisho, Mungy ametoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuitumia mitandao hiyo kwa maendeleo na sio vinginevyo.

“Mitandao hii ya kijamii kama mawasiliano ni maendeleo. Matumizi ya mitandao sio mabaya ila watumiaji ndio wanafanya vitu vibaya. Ningewataka watanzania ambao wanatumia mawasiliano haya vibaya waache. Tuitumie vizuri. Na wale watu ambao unawaona wewe hawaendani na matumizi ambayo yanapendeza, wafute kwenye mtandao wako. Wa-Unlike, wa-Unfriend au wa-delete kabisa ili usione hayo mambo yao ya kipuuzi wanayofanya.”

TUNAISHA TU>>AJALI YAUA WAWILI SONGEA

Wananchi wakiwatoa baadhi ya majeruhi katika basi la Super Feo lililopata ajali Songea.
Miili ya watu wawili waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
WATU wawili wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya ajali mbaya iliyotokea leo huko Songea mkoani Ruvuma ikilihusisha basi la Super Feo linalofanya safari zake kati ya Songea - Makambako lililoacha njia na kugonga mti. Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendo kasi

MBUNGE WAKO VIPI??MBUNGE MGIMWA ASEMA AMETUMIA ZAIDI YA TSH MILIONI 68 KWA MIENZI MITATU YA UBUNGE WAKE KUTEKELEZA AHADI .


Mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa  (kulia) akikabidhi ahadi ya bati 100 alizokuwa ameziahidi mbunge aliyepita marehemu Dr  Wiliam Mgimwa kwa  viongozi wa kijiji cha Mangalali kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa  shule ya msingi Lukwambe hadi  sasa ni asilimia 90 ya ahadi binafsi za mbunge aliyefariki  zimetekelezwa jimbo la Kalenga na mbunge Mgimwa
mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea  ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Diwani wa kata ya Ulanda kulia  akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Mgimwa  kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Katibu  wa mbunge Mgimwa kulia Bw Martine Simangwa  kulia akiteta jambo na mbunge Mgimwa 
Mwananchi  wa kijiji cha Mangalali akisalimia na mbunge wa jimbo la Kalenga  Bw Godfrey Mgimwa
Mbunge Mgimwa akidua sanjari na  wananchi wa kijiji cha Mangalali 
Mmoja kati ya  wananchi wa kijiji cha Mangalali akimpongeza mbunge Godfrey Mgimwa kwa  utendaji kazi mzuri 
Katibu wa Mgimwa akiwaonya  wana CCM wanaojipitisha  jimboni kwa  sasa 
Baadhi ya Wananchi wa  kijiji  cha Mangalali  wakiwa katika mkutano wa mbunge wao Bw Mgimwa



Mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa kulia akikabidhi mchango wake wa Tsh 250,000 kwa ajili ya kusaidia kazi ndogo ndogo  za ujenzi wa zanahati ya kijiji cha Mangalali 
 ........................................................................................................

MBUNGE   wa  jimbo  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa  ajipongeza kutumia kiasi cha  zaidi ya Tsh milioni 68 kwa ajili ya  kufanikisha  utekelezaji wa ahadi  zilizotolewa na mbunge  aliyefariki Dr  Wiliam Mgimwa  kwa  asilimia 90 kwa  muda  wa  miezi mitatu pekee .

Akizungumza na  wananchi  wa  kijiji  cha Mangalali   baada ya  kukamilisha ahadi ya bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lukwambe , mbunge Mgimwa  alisema  kuwa alianza  kutekeleza  ahadi hizo hata kabla ya  kuapishwa   bungeni na  hadi sasa  bado asilimia 10 pekee ya utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge  aliyefariki  dunia mwanzoni mwa mwaka  huu marehemu Dr Mgimwa ambae alikuwa ni babake mzazi.

" Ni jambo la kumshukuru  mwenyezi Mungu  kwani ahadi  zilizokuwa  zimetolewa na  mbunge  aliyefariki  dunia marehemu Dr  wiliam Mgimwa  zilikuwa ni asilimia 100 na hadi mnanichangua  kuwa  mbunge ahadi  hizo  zilikuwa  bado kutekelezwa na ndio  sababu ya mimi   katika kampeni kutoahidi  ahadi mpya  zaidi ya  kuzipokea  zile  zilizoachwa na baba ambazo  kimsingi nilizipokea .......ila kwa sasa ahadi  hizo nimetekeleza kwa asilimia 90  bado asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani  nitakuwa nimezimaliza kikubwa naomba mzidi kuniombea  uzima" alisema  mbunge Mgimwa.

Alisema  kuwa hakuweza  kuahidi ahadi mpya  wakati wa kampeni  hizo za uchaguzi mdogo  jimboni humo kutokana na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo  zilikuwa zimetolewa na mbunge  aliyepita na zilikuwa bado  kutekelezwa na muda  wa   utekelezaji  ulikuwa bado  hivyo aliamua  kuzichukua  zote kama  zilivyo na kuanza  kuzifanyia kazi moja baada  ya nyingine .

Mbunge Mgimwa alisema  kuwa ahadi  hizo  zinazotekelezwa  ni  zile ahadi  binafsi ambazo mbunge  aliyepita alikuwa amezitoa ila  zipo ahadi mbali mbali ambazo zimo katika ilani ya  CCM ambazo pia  zimeendelea  kutekelezwa  kwa  nguvu  kubwa .

Hata  hivyo  alisema kuwa ahadi ambazo  zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja  na elimu ,afya na  uchangiaji wa  vikundi  vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa  vikundi  hivyo pia katika  sekta ya  michezo na huduma  nyingine  za kijamii kama  upelekaji wa umeme katika maeneo ya kata ya Mgama  na Magulilwa zoezi hilo  linaendelea ambayo   ahadi  hiyo ya umeme  ipo katika ilani ya CCM pamoja na zile za  huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi kata ya Maboga  na kata ya Lumuli wa maji  unatekelezwa .

Pia  alisema  kuwa bado  anautamani  ubunge wa  jimbo  hilo la Kalenga kwa mwaka 2015 -2020   hivyo kamwe hatawaangusha  wana Kalenga kwa  kipindi  hiki  cha miaka miwili alichopewa  hadi 2010.

" Ndugu  zangu hii nafasi ya  ubunge  mimi  nimeipata mwishoni ila sikutaka  kuwaangusha  nilitaka kuwaonyesha  utendaji  wangu na kamwe  sitakuwa mbali na ninyi  wananchi  wangu  nitakuwa  bega kwa  bega  kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata maendeleo na linakuwa ni  jimbo la mfano katika maendeleo  kule  bungeni kutokana na umri  wangu  wabunge  wananiita bwana mdogo ila  kiutendaji kweli  ni bwana mkubwa kwani kati ya wabunge zaidi ya 300 bungeni  mimi ni mmoja kati ya  wabunge  tuliochanguliwa  kuingia katika kamati ya bunge ya bajeti ya  serikali " alisema mbunge Mgimwa .

Awali katibu  wa mbunge huyo  Martine Simangwa  aliwaonya  wana CCM ambao  wameendelea  kujipitisha katika  jimbo  hilo na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki  wananchi wa  jimbo la Kalenga ambao kwa  sasa wameshikamana na  wapo tayari kuona  maendeleo na sio kampeni za  uchaguzi wa mwaka 2010.

"  wapo  baadhi ya  wana CCM bila haya  wameendelea  kujipitisha kwa wananchi na  kuponda utendaji huu mzuri wa mbunge Godfrey Mgimwa ....sasa  wananchi  nawaombeni  sana msidanganyike na  watu hao kwa sasa mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na kuwapa  pesa chukueni ila msikubali kugawanywa kwa misingi ya pesa kubalini  kuungana katika misingi ya kimaendeleo"

Kwa upande  wao  wananchi hao  walieleza  kufurahishwa na utendaji mzuri wa mbunge  wao Mgimwa na  kuwa kamwe hawatakubali kudanganyika na kuwa  wamejipanga  kumchukulia  fomu mwakani  ili kuwaongoza vipindi  vingine viwili zaidi baada ya  kuona utendaji  wake mzuri.

MWISHO

Snura mezani kwa Soudy Brown,kuhusu stori zinazosema kuwa ni mjamzito.

snuraaa
Kupitia singo zake za Majanga,Nimevurugwa na Ushaharibu zimefanya Tanzania na nje ya Tanzania kumfahamu Snura ambaye style ya muziki wake na namna ambavyo anaperfoam on stage imemfanya kuwa na mashabiki wengi.
Mezani kwa Soudy Brown kuna  stori ambazo zimesambaa kuwa Snura ni mjamzito ndiyo sababu inayomfanya kutosikika vizuri kama mwanzo,Meneja wake HK amezungumzia hili,baada ya Snura mwenyewe kutopatikana.

Rais Jonathan - mabango yang'olewe(BRINGBACKJONATHAN)

Harakati za kampeni nchini Nigeria
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamuru mabango ya hekeheka za uchaguzi yenye nembo ya kauli mbiu ya 'Bring Back Jonathan 2015' yang'olewe mara moja.
Mabango hayo yamelaaniwa vikali kwenye mitandao ya kijamii kwani yanaonekana kuiga kauli mbiu iliyotumiwa katika kampeini ya kuitaka serikali kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram mwezi Aprili mwaka huu.
Kundi hilo la wapiganaji wa kiisilamu bado linawashikilia wasichana hao, Wakati ambapo mabango ya Bring Back Jonathan 2015 yaliowekwa kando ya barabara kuu mjini Abuja, yalilaaniwan vikali nchini Nigeria na kimataifa kupitia katika mitandao ya kijamii.
Watu walihisi kuwa ilikuwa ni kama kejeli kwa kampeini ya 'Bring Back Our Girls' ambayo ilienea kote duniani baada ya Boko Haram kuwateka nyara wasichana wa shule ya Chibok.
Wasichana hao 219, bado hawajulikani waliko miezi mitano baada ya kutekwa kwao.
Rais Jonathan, ameyataka mabango hayo kuondolewa kwenye barabara za mji haraka iwezekanavyo.
Katika taarifa yake alisema yeye pamoja na wanigeria wengi wanahisi kuwa kampeini hiyo ilikuwa na nia mbaya na kusisitiza kuwa juhudi bado zinafanywa kuwoakoa wasichana hao waliotekwa na Boko Haram.

WEMA CHUNGA SUKARI YAKO::ANTI LULU: ATAKA KUZAA NA DIAMOND

Stori: Waandishi Wetu
MOYO unahifadhi mengi! Msichana wa mjini asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ amefunguka kwamba yupo tayari kuzaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwani amepata taarifa kwamba anasaka mtoto lakini wanawake anaokuwa nao hawataki kumzalia, Ijumaa Wikienda linakupasha.
Msichana wa mjini asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ akipozi.
BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada azae naye.
MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).
“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” alisema Anti Lulu.
Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na Diamond.
Mkali wa Bongo Fleva 'Diamond Platinum' akiwa na mpenzi wake wema Sepetu.
IMANI
Anti Lulu alisema kwamba anaamini Diamond atamkubali japokuwa hawajawahi kuzungumzia hiyo ishu wakiwa pamoja na kwamba walishakutana na kuzungumza mambo mengine.
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii...
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?
MTOTO MZURI
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya Kinondoni halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba aliponiona siku hiyo alinisifia.
“Niliambiwa alisema kwamba mimi ni mwanamke mzuri na umbo langu ni zuri hivyo naomba akubali tu nimzalie jamani,” alisema Anti Lulu ambaye aliwahi kuwa prizenta wa runinga na mwigizaji wa sinema za Kibongo.
BIFU?
Anti Lulu alidai kwamba japokuwa anaamini kabisa kwamba Wema atakasirika, hatajali kama mbwai iwe mbwai na yupo tayari kuanzisha naye bifu zito.
'Diamond Platinum' wakati akiwa na Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Alisema kila mmoja atakuwa na nafasi yake kwa Diamond na kwamba kikubwa anataka kuzaa na Diamond halafu amkabidhi mtoto kila mmoja aendelee na maisha yake.
NENO!
“Najua Wema atakuwa na bifu na mimi lakini sijali kwa sababu nimeamua na yeye ni mpenzi wa Diamond tu siyo mke wake kwani hawajafunga ndoa.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.
DIAMOND, WEMA NA PENNY
Diamond aliwahi kuripotiwa kumpa ujauzito aliyekuwa mpenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ lakini baada ya muda mfupi ilidaiwa kuchoropoka.Pia aliwahi kudaiwa kumpachika kibendi Wema ambaye naye ilidaiwa ilichoropoka.
Kwa upande wake Anti Lulu aliwahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Bond Bin Sinan na Amani ambao hakufanikiwa kuwazalia watoto.
SWALI LENYE HOJA!
Baadhi ya watu waliomsikia Anti Lulu akitangaza ishu hiyo walijiuliza swali moja tu: ‘Hivi kweli Anti Lulu huyuhuyu anaweza kuwa mama bora?’Diamond hakupatikana ili kufikishiwa ujumbe huo na kujua namna alivyopokea taarifa hiyo ya Anti Lulu.

PAMOJA NA JUHUDI ZAKE::KIJANA AUAWA AKITUHUMIWA USHIRIKINA

Marehemu akipakiwa kwenye gari tayari kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti.
Ndugu na jamaa wakishiriki maziko ya marehemu,  Gabriel Mwasyebule kijijini kwao ndembo lwangwa.
Marehemu Gabriel Mwasyebule enzi za uhai wake.

Nyumba ya marehemu, Gabriel Mwasyebule anayotuhumiwa kuijenga kwa uchawi.
Moja ya shamba la viazi vinavyo subiriwa kuvunwa mwezi huu, shamba la marehemu, Gabriel Mwasyebule, mashamba amabayo pia ni moja ya sababu ambazo wananchi wa lwangwa wanamtuhumu marehemu kuwa alikuwa anawalimisha watu kiuchawi na kuiba mazao ya mashamba mengine kiuchawi ili shamba lake liwe na mazao mengi na mazuri.
Hii ndio stoo kuwekea mazao mbalimbali ambayo marehemu alikuwa anatumia kutunzia mazao yake.
MATUKIO ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio hili kijana Gabriel Mwasyebule miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja marehemu aliyetambulika kwa jina la Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande (Lwangwa) Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kifuani.

Alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumapili majira ya saa tano asubuhi huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoaniMbeya

Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo uliitisha kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.

Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi ya mavuno ya viazi na kujipatia pesa zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake aliyoweka marumaru na Gipsam pia kumiliki pikipiki moja huku akitarajia baada ya mavuno mazuri ya mwaka huu kununua gari la kutembelea.
Chanzo: Jamiiforums

KUDADADEKIII:::HUYU MKULIMA JEURI SANA AAMUA KUTEMBEZA BATA 5000 BARABARANI

 














mkulima mmoja wa nchini china akiwa na bata wake idadi ya 500, akidai anawafanyisha mazoezi barabarani

IT'S the kind of sight that would stop any traveller in their tracks.
A Chinese farmer brought traffic to a standstill when he took his flock of 5000 ducks out for a stroll to a nearby pond.

Armed with only a cane, the man and a colleague took the feathered friends on the walk of about 1km as part of an annual tradition in Zhejiang province.

The farmer claims that not one of the ducks was lost in transition during the tricky duck migration manoeuvre.
Ducks in Taizhou, China
Taizhou is about 300km south of Shanghai and has a population of almost six million.

Other tourist drawcards include Linhai Ancient Great Wall - the only Great Wall in southern China - Tiantaishan National Park and the Tiantaishan Temple, which is the birthplace of an important school of Buddhism throughout Asia.

VITUKO VYA LEO::PICHA ZA KUKU MWEUSI KULIKO WOTE DUNIANI