Friday, 17 October 2014

MAMBO YA NDOA::NINI CHA KUFANYA MUMEO ANAPOZAA NJE YA NDOA?

Nianze kwa kumshukuru Mungu ambaye ameniweka hai mpaka siku hii ya leo, tunapokutana tena kwenye uwanja wetu huu kujuzana, kujadiliana, kuelimishana na kuzungumzia ishu mbalimbali zinazohusu uhusiano wa kimapenzi.
Leo nataka kuzungumza na wewe mama, dada, shangazi au mwanamke ambaye upo kwenye uhusiano wa kudumu, nikimaanisha umeolewa. Je, umewahi kugundua, kuhisi au kuambiwa kwamba mumeo mliyeishi pamoja kwa kipindi kirefu, amezaa mtoto na mwanamke wa nje?
Bila shaka kila mmoja atakuwa na majibu yake lakini katika mada hii nataka kuzungumza zaidi na wahusika, wanawake ambao wamewahi kutokewa na tatizo hili. Ni ukweli usiofichika kwamba wanaume wengi siku hizi wamekuwa na mchezo wa kuzaa nje ya ndoa.
Yaani amekuoa na mnaishi pamoja kama mume na mke, mmejaliwa kupata mtoto au watoto lakini kumbe nyuma ya pazia, yupo mwanamke mwenzako ambaye naye amezalishwa na mumeo. Je, unapaswa kufanya nini katika mazingira kama haya?
Mada ni nzito na ndiyo maana napenda zaidi kusikia kutoka kwa waliotokewa na tatizo hili kwani naamini kupitia wao, wengine watajifunza na hata watakapokuja kutokewa na hali kama hii, watajua namna ya kupambana nalo.
Je, ukigundua mumeo ana mtoto nje ya ndoa, utadai talaka, utamtafuta mwizi wako mpaka umpate na kumshikisha adabu, utamsaka mtoto ili umdhuru au utafanya nini? Hebu sikiliza ushuhuda wa mwanamke huyu ambaye nimewahi kukutana naye, akanisimulia mkasa wake ambao leo ndiyo ulionisukuma kuja na mada hii.
“Mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa miaka minne iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Wa kwanza ana miaka mitatu na huyu mwingine bado hajafikisha hata mwaka mmoja. Mume wangu ni mfanyakazi wa kampuni moja kubwa jijini Dar es Salaam.
Kwa kipindi chote tangu tuoane, tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo wa hali ya juu mpaka miezi michache iliyopita ambapo nimegundua jambo baya mno katika ndoa yangu.“Nimegundua kwamba mume wangu ana mtoto mwingine ambaye ana umri wa miaka miwili.
Huyo mwanamke aliyezaa naye, mwanzo walikuwa wakifanya kazi pamoja ingawa sasa nasikia hayupo tena kazini kwa mume wangu ila nimesikia tetesi kwamba mume wangu ndiye aliyempangia chumba na anamhudumia kila kitu na siku nyingine huwa anaenda nyumbani kwake.
Nipo njia pandaa najihisi nakaribia kupatwa na ugonjwa wa moyo, ndoa yangu naiona chungu, namchukia sana mume wangu japokuwa ameniomba msamaha, sidhani kama nitamsamehe, naomba ushauri, nifanyeje?”
Hayo ndiyo maelezo aliyonipa mwanamke huyo ambaye kiumri bado ni mbichi na ndoa yake ndiyo hiyo ina miaka minne. Mpendwa msomaji wangu, bila shaka umeyaelewa vizuri maelezo ya dada huyu na tayari unayo majibu ya kumpa. Je, utamshauri nini?
KOSA LA MSINGI
Kosa la msingi ambalo mume wa dada huyu alilifanya ni usaliti. Yaani licha ya mwenzake kumpenda kwa moyo wote, aliamua kuchepuka na kwenda kwa mwanamke mwingine na kumpa ujauzito, kosa juu ya kosa.
Kosa la usaliti pekee ni baya na kama tulivyowahi kuzungumza kipindi cha nyuma, humchukua muda mrefu sana mtendewa wa usaliti kurudi kwenye hali yake ya kawaida na kurejesha mapenzi kwa aliyemtenda. Wengine hujikuta wakishindwa kabisa kusamehe na kusahau yaliyotokea.
Inapotokea usaliti umesababisha mtoto wa nje, uzito wa kosa huwa mkubwa zaidi na hata namna ya kulishughulikia, ni lazima wanandoa wote wawe makini sana kwani vinginevyo, huo unaweza kuwa mwisho wa ndoa au mapenzi kati ya wawili hao.

AFRIKA::Liberia yaelemewa mapambano dhidi ya Ebola


ebola-virus-393486
Wakati ulimwengu ukikabiliwa na changamoto ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa Ebola, nchi ya Liberia ambayo imeathiriwa zaidi na ugonjwa huo imetangaza kukabiliwa na upungufu wa mifuko maalum ya kubebea miili ya marehemu waliofariki kwa Ebola.
Serikali ya Liberia imesema kwa sasa ina takribani mifuko 4,900 tu, ikilinganishwa na idadi ya zaidi ya mifuko 85,000 inayohitajika ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.
Takwimu zinaonesha uhaba mkubwa wa vifaa muhimu katika kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na suti za kujikinga, kifaa maalum cha kujikinga uso, glavu, miwani pamoja na mifuko ya kubebea maiti.
Imeripotiwa kuwa Liberia itahitaji boksi milioni 2.4 ndani ya kipindi cha miezi sita, huku kiasi kilichopo kwa sasa ni boksi 18,000, na kwa upande wa idadi ya kofia zinazohitajika ni milioni 1.2 na kwa sasa inaripotiwa kuwa ziko 165,000. Uhaba huo unatajwa kama kikwazo kikubwa katika kukabiliana na ugonjwa huo ambapo katikati ya wiki hii kuliripotiwa mgomo wa wauguzi wakidai nyongeza ya mshahara.
Tangu kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola mwezi wa tatu mwaka huu, takribani watu 9000 wameripotiwa kuathirika, na wengine zaidi ya 4,000 wameripotiwa kupoteza maisha katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani, huku zaidi ya nusu ya vifo hivyo vikiripotiwa kutokea nchini Liberia.
Taarifa ya shirika la afya duniani (WHO) imetahadharisha kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi siku za usoni katika mataifa hayo matatu na kupelekea idadi ya waathirika kuongezeka na kufikia 10,000 kwa wiki hadi itakapofikia mwisho wa mwaka.
Liberia inatarajia kupokea vifaa mbalimbali wiki ijayo ikiwemo mifuko ya kubebea maiti, lakini taarifa ya shirika hilo inaongeza kuwa vifaa hivyo bado havitoshelezi kukidhi hali ya uhitaji iliyopo katika nchi hiyo.
Mbali ya nchi hizo tatu zinazotajwa kuathiriwa zaidi na ugonjwa wa Ebola, nchi nyingine zilizotajwa kuripotiwa kukumbwa na janga la ugonjwa huo ni pamoja na Senegal, Nigeria, Hispania na Marekani.

SKENDO KENYA::Wanariadha watumia sana madawa Kenya

Ripoti kuhusu utumizi wa madawa ya kusisimua misuli michezoni, miongoni mwa wanamichezo nchini Kenya, imebainisha kuwa idadi kubwa ya wanariadha wa Kenya wanatumia madawa hayo yaliyoharamishwa.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hii leo na waziri wa michezoi nchini Kenya, jumla ya wanamichezo thelathini na saba kutoka Kenya wamepatikana na hatia na miongoni mwa michezo iliyoathirika zaidi ni riadha, raga, soka, unyanyuaji wa uzani na table tennis.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya uchunguzi Profesa Moni Wekesa amesema tatizo hilo ni kubwa na linahitaji suluhisho la haraka.Amesema miongoni mwa madawa yanayotumiwa zaidi ni bangi, mirraa na 'Steroids.'
Aidha ripoti hiyo imenadi kuwa makocha na meneja wa kigeni ndio wanaowapa wanariadha madawa hayo ili kuandikisha matokeo bora katika mashindano ya kimataifa.
Waziri wa Michezo nchini Kenya, Hassan Wario naye ameilaumu shirikisho la mchezo wa riadha nchini kwa kutowajibika.
 
Waziri wa michezo nchini Kenya Hassan Wario
Kati ya wanamichezo 37 waliopatikana na hatia ya kutumia madawa hayo yaliyoharamishwa 31 ni wanariadha.
Hata hivyo waziri huyo amesema baadhi ya wanariadha hao walitumia madawa hayo bila kujua, akitoa mfano wa mwanariadha Lydia Cheromei ambaye alipigwa marufuku kwa muda licha ya kuwa alikuwa amepewa dawa za uzazi na wala sio dawa ya kuongeza nguvu.
Shirikisho la riadha nchini humo pia limeshutumiwa kwa kutoimarisha mikakati ya kupambana na utumizi wa madawa hayo, kwa kutoa mafunzo kwa wanariadha wake na pia kwa kutoa vibali vya kuwaruhusu mawakala wa kigeni kupiga kambi nchini humo, bila kufuata masharti yaliyopo.
Kinyume na taasisi zingine za michezo, shirikisho la riadha nchini Kenya lilisusia uzinduzi wa ripoti hiyo, hali iliyozua shaka kuwa huenda wao hawaiungi mkono.
 
Waliosemekana kutumia zaidi dawa za kusisimua misuli ni wanariadha
Mbali na wanariadha, wachezaji wa soka, pia walishutumiwa kwa kutumia miraa na bangi. Mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya, Sam Nyamweya amekiri kuwa wachezaji wengi wa timu ya taifa na wale wanaoshiriki ligi kuu baadhi yao huvuta bangi kabla na baada ya mechi.
Wakati huo huo serikali ya Kenya imetangaza mpango wa kubuni shirika maalum litakalokuwa na jukumu la kupambana na utumizi wa madawa ya kusisimua misuli michezoni.
Waziri wa michezo amedokeza kuwa shirika hilo litashirikiana kwa karibu na shirika la kimataifa la WADA, kujenga kituo maalum ambacho kitatumia kupima sampuli za wanamichezo wote.
Kuhusu usajili wa maagenti wa kigeni, serikali imeipokonya shirikisho la mchezo wa riadha nchini kenya, idhini ya kutoa leseni na badala yake, maagenti wote wa kigeni watalazimika kutuma maombi yao upya kwa wizara ya michezo, kabla ya kuruhusiwa kufanya kazi.

NI SHEEDAH:::Maandalizi ya mwisho ya Jukwaa la Serengeti Fiesta Dar es salaam.

8stg
Baada ya kupita mikoa mbalimbali ya Tanzania sasa imefika zamu ya wakazi wa Dar es salaam kuonja utamu huu wenye msimu wa mafanikio ndani yake sehemu moja ambayo tutakusanyika wote.
Leaders Club ndiye sehemu pekee iliyoteuliwa kuwapokea wakali mbalimbali akiwemo Waje kutoka Nigeria,Victoria Kimani kutoka Kenya,T.i na wasanii wengine ambao watakua kama surprise kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dsm.
Jukwaa tayari limekamilika kwa asilimia zaidi ya 80 na wasanii mbalimbali leo wataanza kulifanyia mazoezi kabla ya shughuli yenyewe ambayo ni kesho Oct 18,kiingilio ni 15,000 ukinunua kabla na 25,000 pale Getini.
Baadhi ya picha za hili jukwaa la Serengeti Fiesta Dar es salaam.
13stg
12stg
10stg
9stg
11stg

13stg

8stg
10stg
8stg
7stg
6stg
5stg
5stg
25stg   21stg    16stg
19stg

MAHAKAMANI::Wakili asema Pistorius 'amefilisika'


Inaarifiwa Pistorius ametumia pesa zake kwa kesi inayomkabili
Mahakama inayosikiliza kesi dhidi ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeambiwa kuwa mwanariadha huyo amefilisika.
Hili lesemekana huku pande zote kwenye kesi zikitao akuli yao ya mwisho kabla ya mahakama kutoa hukumu dhidi ya mwanariadha huyo.
Pistorius alipatikana na hatia ya mauji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp bila ya kukusudia mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya Pistorius Jumanne.
Anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 lakini jaji anaweza kuamua kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza faini.
Jaji ataanza kusoma hukumu Jumatatu na upande wa mashitaka unataka Pistorius apewe adhabu kubwa kuambatana na kosa lake.
 
Pistorius aliangua kilio wakili wake alipoambia mahakama kuwa amefilisika
Lakini mawakili wa Pistorius wameteta wakisema anapaswa kupewa adhabu ndogo kama vile huduma kwa jamii.
Wanadai kuwa mwanariadha huyo huenda akateswa akiwa jela, hoja ambayo imepingwa vikali na mkuu wa magereza.
Pistorius aliangua kilio wakli wake aliposema kuwa pesa zake zimekwisha baada ya kesi yake kufanya kwa mirzi saba.
"sio tu kwamba hana pesa bali anahisi hana tena matumaini,'' alisema wakili wa Pistorius.
Hii ni kesi yake ya kwanza. Nini kimtendekea mwanamume huyu? Nyota yake ilikuwa inaanza kung'ara,'' aliongeza bwana Roux.
Wakili alimuomba jaji kumuonea huruma Pistorius wakati atakapotoa hukumu.
Mnamo siku ya Ijumaa, kiongozi wa mashitaka alikosoa pendekezo la Pistorius kuikabidhi familia ya Reeva pesa. Hata hivyo familia ya Reeva ilikataa pesa hizo ikisema ni pesa za uovu.
Bwana Nel pia alisema ikiwa Pistorius atapewa adhabu ya kiungo cha nje na kuamrishwa kuihudumia jamii, itakuwa ni hujuma kwai adhabu hiyo itakuwa ndogo sana kulingana na kosa lake.

GUMZO MITANDAONI::Mwanasiasa aliyeahidi kula saa yake

Ni bora kuwa mwangalifu hasa kuhusu kile unachoahidi watu maana yanaweza ya kukuta kama yaliyomkuta mwanasiasa mmoja nchini Bolivia.
Mwanasiasa huyu Jorge "Tuto" Quiroga, alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi uliokamilika Jumapili iliyopita nchini Bolivia.
Rais huyo wa zamani ambaye pia alikuwa mpinzani mkuu wa Rais Evo Morales alitoa ahadi moja ambayo ikiwa angejua matokeo kabla ya uchaguzi basi asingedhubutu kuitoa.
Ilikua ahadi ambayo haikuwa na busara.
Aliahidi kukula saa yake ikiwa kila wabolivia 'sita' kati ya 'kumi' wangempigia kura Rais Morales.
 
Jorge "Tuto" Quiroga aliahidi kula saa yake na tai ikiwa Morales angepigiwa kura kwa wingi
Alikuwa na uhakika sana kuwa Morales asingeweza kushinda uchaguzi kiasi cha kutoa ahadi nyingie ya kutatanisha ya kula tai yake katika mahojiano mengine siku chache zilizofuata.
Na sasa mitandao ya kijamii nchini Bolivia Facebook na Twitter imejaa taarifa za wananchi kumtaka mwanasiasa huyo atimize ahadi zake. Mwanzo ale saa yake na kisha afuatie ne tai yake.
''Je ni lini ambapo Tuto Quiroga atakula saa yake?'' alihoji mtu mmoja.
Tuffi Aré, mtumiaji maarufu wa Twitter alimhoji bwana Quiroga kabla ya uchaguzi mkuu. Yeye alituma ujumbe kwa Twitter akisema labda bwana huyo anasubiri matokeo kamili ya uchaguzi ndipo ale saa yake.
Pia alihidi atakula Tai yake na yote hayo yalinakiliwa.
Ingawa watu wengi nchini Bolivia wametoa maoni yao kwenye Twitter na Facebook, wengi wanaomshinikiza mwanasiasa huyo ni wafuasi wa Rais Evo Morales aliyeibuka mshindi wa uchaguzi huo.

FIESTA DAR::Davido ndani ya Dar es salaam tayari! picha 7 ziko hapa

12
Sina Rambo ni mshkaji wa long time wa Davido.
Pale ambapo unakutanishwa na miongoni mwa mastaa wanaofanya vizuri kwenye list ya hits za Afrika kwa sasa…….. pale ambapo pia unapewa ruhusa ya kuona akifanya yake kwa zaidi ya dakika 20 mbele ya macho yako.
11
13
10
9
7
5
Mussa Mateja mwandishi wa Global Publishers akiwa na Davido.

TANZANIA::BIG RESULT NOW(BRN)...AGE is a number.......

Miss TZ
Kama ulifatilia shindano la Miss Tanzania 2014 weekend iliyopita utakua unajua kilichotokea na kinachoongelewa ikiwa ni baada ya baadhi ya watu kupinga au kutoridhishwa na matokeo ya mshindi aliyetangazwa ambae ni Sitti Mtemvu mtoto wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu.

Ebola:Annan akosoa mataifa ya Magharibi

Annan anasema hajaridhishwa na juhudi za mataifa ya magharibi kupambana na Ebola
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amekosoa ambavyo mataifa ya magharibi yameshughulikia janga la Ebola.
Bwana Annan ameambia BBC kwamba hajaridhishwa kamwe na hatua za mataifa ya magharibi kupambana na Ebola.
''Ikiwa janga hilo lingekuwa limeathiri eneo lengine , hatua ambazo zingechukuliwa zingekuwa toifauti sana.''
''Hata ukiangalia ambavyo janga hili limekuwa likienenea , mataifa ya magharibi yalichukua hatua tu wakati ambapo ugonjwa huo ulitambuiliwa katika mataifa yao kama vile Marekani na Ulaya.''
Kwiengineko, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezindua kampeini ya kuchagisha mamilioni ya dola kusaidia kwa vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola, baada ya kampeini ya awali ya kuchangisha pesa kukosa kufikia malengo yake.
 
Ban Ki-Moon anaomba ufadhili zaidi katika vita dhidi ya Ebola
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kampeini aliyozindua mwezi Septemba kuchangisha pesa imefanikisha tu mchango wa dola 100,000 kufikia sasa.
Ban Ki Moon ni mmoja wa viongozi wa kimataifa wanaokosoa juhudi za kimataifa za kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola akisema ni hafifu mno.
Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 4,500 kufikia sasa wengi wakiwa katika mataifa ya Liberia, Guinea na Sierra Leone.
Wadhamini wametoa mchango wa karibu dola milioni 400 kwa mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa lakini sio kwa kampeini aliyozindua bwana Ban ambayo inapaswa kuwa kama akiba ya pesa zitakazotumiwa kwa vita dhidi ya Ebola pindi zinapohitajika.

Kuna ahadi ya dola milioni 20 katika mchango zitakazotolewa kwa kampeini hiyo.
Kati ya mataifa ambayo yameahidi kutoa mchango wao kwa Ban Ki Moon ni Colom,bia pkeke ambayo tayari imetoa dola laki moja.
Mjumbe maalum wa Umoja huo kuhusu Ebola, David Nabarro, amesema hazina hiyo itakuwa afueni kwa vita dhidi ya Ebola ambavyo kwa sasa limegeuka na kuwa janga la kimataifa.
Bwana Ban amesema ni wakati kwa dunia nzima kuchukua hatua haya mataifa yenye uwezo mkubwa kutoa msaada wa kifedha na uwezo wa kuwafikia wagonjwa na pia kutoa matibabu.
Wito kama huo umetolewa katika siku za hivi karibuni na Rais wa Marekani Barack Obama , waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim.

UFAHARI:: Ni staa gani wa bongofleva kaamua kuweka jina badala ya namba kwenye gari lake? picha iko hapa


bmw 2
Ni wiki zinahesabika toka staa wa bongofleva Nay wa Mitego apate namba mpya ya gari lake inayoendana na ile ambayo amekua akiitaja kwenye nyimbo zake na kwenye page zake za mitandao ya kijamii. #966
Stori nyingine ya leo ni kutoka kwa staa mwingine wa bongofleva ambae kila anaefatilia huu muziki hapa bongo anamfahamu, ni yuleyule ambae amevunja rekodi ya kuwa staa pekee wa Tanzania alieandikwa sana kwenye mitandao ya kijamii na magazetini kwa miaka miwili mfululizo.
Ni Diamond Platnumz ambae kwenye birthday yake hivi karibuni management yake ilimzawadia gari aina ya BMW X 5 ambapo inaaminika amechukua namba hizi kwa ajili ya mkoko wake aliozawadiwa……….. atakua msanii wa kwanza kuweka jina lake badala ya namba kwenye gari.
Utaratibu wa kuweka majina badala ya namba umeanza kutumika kihalali nchini Tanzania ambapo watu mbalimbali wasio maarufu walishaanza kujiwekea miezi kadhaa iliyopita ambapo ada yake ni milioni tano kwa miaka mitatu.
Platnumz
Mpango wa mastaa kuweka majina kwenye magari yao badala ya namba tulizozizoea umekua ukitumika kwenye nchi mbalimbali duniani ambapo kwa Afrika Mashariki Uganda ndio inaongoza kwa kuwa na mastaa wengi waliotundika majina kwenye mikoko yao.
D
Gari alilozawadiwa Diamond kwenye birthday yake.

SKENDO LA SITTI::Baada ya Miss TZ 2014 kuandamwa mitandaoni, Miss TZ wa 2013 ameamua kuyaandika haya

Brig
Kama na wewe unakerwa au haupendi jinsi ambavyo Miss Tanzania wa 2014 Sitti Mtemvu amekua akiandamwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu umri wake na elimu yake baada ya kushinda taji hilo weekend iliyopita basi uko upande mmoja na Miss Tanzania wa 2013 Brigitte Alfred.
Kupitia page zake za twitter na Instagram Brigitte pamoja na mengine ameandika >>> ‘ Mazuri mengi yanawapita lakini inapotokea skendo mnajadili milele ndio maana hatuendelei, natamani tungeweka hizi nguvu za matusi kwenye vitu vya kujenga‘
Baada ya hiyo sentensi Brigitte alimuandikia Sitti kwa kusema >>> ‘Sitti usiwaruhusu watu wakuandame sana, ikizidi warudishie tu taji lao’
Miss Tanzania Brigitte
Kwenye tweets nyingine za wiki hii baada ya Sitti kutangazwa mshindi Brigitte aliandika ‘mngejua siasa za huko Miss World hata msinge jisumbua kumshambulia huyu msichana kiasi hicho, mtihani wa Miss Tanzania sio tu siku ya fainali ndio maana kunakua na camp ya siku 30′
Miss Tanzania 1
Miss TZ 3
Miss TZ 2

MSUMBIJI::Renamo-hatutambui matokeo



Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO,kimetoa yake ya moyoni kuwa hawatayakubali matokeo yajayo ya uraisi na ubunge pamoja na serikali za mitaa.
Msemaji wa chama hicho Antonio Muchanga amesema kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu katika upigaji kura huo na udanganyifu wa kura.
Matokeo ya awali katika uchaguzi huo zinaonesha kwamba chama cha FRELIMO kinaongoza katika uchaguzi huo.Wakati haya yakitokea kumekuwa na uvunjifu wa amani wakati polisi walipo ingia katika ghasia na waandamanaji waliokusanyika nje ya vituo vya kupigia kura kufuatilia zoezi la uhesabuji wa kura .
Ingawa wafuatiliaji wa uchaguzi nchini Zimbabwe wanaeleza kuwa pamoja na yote hayo,uchaguzi huo ulikua huru na wa haki.ikumbukwe kuwa chama cha Renamo na chas Frelimo walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mnamo mwaka 1982.(BBC)

VITUKO::Rihanna Awashtua Watu Kwa Kubeba Bunduki Hadharani


Rihanna Mwanamuziki Asieisha Vituko Ameamua Kubeba Mkoba Unaofanana Na Bunduki Huku Akijiachia  Nao Hadharani Kitu Ambacho Watu Wamejikuta Wanamshangaa Na Kujiuliza Maswali Mengi Bila Kupata  Majibu Na Sio Mara Ya Kwanza Kubebea Mikoba Inayofanana Na Vitu Vya Aina Mbalimbali