Thursday, 11 September 2014

DOKII AGOMA KUZUNGUMZIA NDOA

Na Gladness Mallya
MWANADADA  anayefanya vizuri kunako gemu la muziki Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ hivi karibuni alinaswa akitoa meno yote nje baada ya kushuhudia sherehe ya msanii mwenzake, Lucy Komba na kusema ya kwake hawezi kuizungumzia kamwe.
Msanii mkongwe wa tasnia ya filamu bongo Ummy Wenslaus ‘Dokii’
Akizungumza na paparazi wetu, Dokii alisema amefurahi sana Lucy kuolewa na Mzungu na alidhani kwamba ni mzee kama Waafrika wengine wanavyopenda kuolewa na Wazungu wazee lakini amempata kijana mzuri anayevutia hivyo ana bahati ya pekee lakini kwa upande wake ndoa hataki hata kuisikia.
“Kuhusu mimi siwezi kuzungumzia na huwa sipendi kabisa kuzungumzia suala la ndoa yangu kama nimeolewa au nitaolewa ila naendelea kumpongeza Lucy kwani siyo msichana yule wa kujisikia wala nini anaongea na kila mtu,” alisema Dokii ambaye hajawahi kumwanika mwanaume wake.

No comments:

Post a Comment