Saturday, 13 September 2014

Hakuna Ubishi Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji Ndio Anaivuruga Klabu Hiyo.


Mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Yusuph ‘Tigana’, amesema Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji (pichani) ‘anaivuruga’ klabu hiyo.

Tigana aliliambia gazeti hili juzi katika mahojiano maalumu kuwa Manji amekuwa akifanya uamuzi aliouita wa kibabe, ambao umekuwa ukichangia kuivuruga timu hiyo.

Winga huyo wa zamani wa Yanga na timu ya taifa (Taifa Stars), alisema Yanga imekuwa ‘ikipelekwapelekwa’ na

kiongozi huyo na kusisitiza kuwa amekuwa akifanya anavyotaka kwenye klabu hiyo huku Wanayanga wakikaa kimya kwa sababu ana fedha.

“Yanga sasa inapotea sababu ya kiongozi mmoja tu, sababu ana fedha, ndani ya klabu kumekuwa na uamuzi ambao si wa wote unafanywa na mtu mmoja kisa ana fedha, hivyo anaamua kufanya anavyojisikia,” alisema Tigana na kuongeza.

“Hata suala la Okwi (Emmanuel) linafanywa kibabaishaji isitoshe mchezaji huyo alistahili kwenda Simba, mimi sioni sababu ya Yanga kuendelea kumng’ang’ania na kutishia kwenda FIFA, lakini kwa kuwa mwenyekiti wetu ana pesa basi anaamua kufanya ubabe

No comments:

Post a Comment