Bunge la China limeazimia kuondoa hukumu
ya kifo kwa baadhi ya makosa ambapo rasimu ya mapendekezo ya
marekebisho ya katiba tayari imewasilishwa katika bunge la nchi hiyo.
Rasimu ya mabadiliko hayo imewasilishwa
kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza katika kikao cha bunge hilo
ambacho kinatarajiwa kukaa kwa muda wa miezi 2.
Katika mapendekezo hayo, makosa ambayo
yametakiwa kuondolewa adhabu ya hukumu ya kifo ni pamoja na kosa la
usafirishaji ama kumiliki silaha na nyuklia kinyume cha sheria, fedha
badhia, kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, kujishughulisha na
biashara ya ukahaba, kumzuia askari au mwanajeshi kutimiza wajibu wake,
na kuzusha uvumi wa uongo wakati wa kupigana vita.
Iwapo mabadiliko hayo yakifanyika, wale
ambao wamekwishahukumiwa adhabu hiyo, watabadilishiwa hukumu na badala
yake kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu zaidi.
China inatajwa kuwa ni moja ya nchi
zinazoongoza kutoa hukumu ya kifo, ambapo taasisi moja ya haki za
binadamu ya Dui Hua imesema kwa mwaka jana peke yake China imehukumu
kifo kwa takribani watu 2,400 huku kukiwa hakuna takwimu rasmi
zilizopatikana mpaka sasa juu ya idadi ya watu wanaonyongwa kila mwaka
nchini humo.
No comments:
Post a Comment