Saturday, 11 October 2014

HABARI::KATIBU MKUU CCM;SINA HABARI NA MSIGWA,KAZI KUTUKANA..

Kinana  akiwahutubia  wananchi wa Iringa mjini leo

KATIBU  mkuu  mkuu  wa   chama  cha mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana awakuna  wananchi   wa jimbo la Iringa mjini   linaloongozwa na mchungaji Peter Msigwa (chadema) kwa  kuwataka  wana CCM kusoma alama  za nyakati badala ya  kuendelea   kutaka kuendelea  kugombea huku  wakijua  wakati  wao wa  kupendwa umekwisha.
Kuwa  rushwa  ndani ya  CCM na  serikali yake ndio ambao inakipeleka pabaya  chama    hicho  pamoja na ugomvi usiokwisha  ndani ya CCM.
Alisema  kuwa tabia ya   baadhi ya  wagombea  kulazimisha  kuendelea  kugombea  huku  wakijua wamechaja ni  moja kati ya  sababu ya  CCM kuendelea  kuchokwa na  wananchi na  hivyo kuamua  kuchagua  wapinzani.
Akiwahutubia  wakazi wa  jimbo la Iringa mjini katika  uwanja wa Mwembetogwa  leo  Kinana  alisema  kuwa tatizo la CCM  kupoteza  jimbo hilo ni uroho wa madaraka kwa  wale ambao  hawakubaliki  kwa wananchi kosa  ambalo kamwe  CCM haitarudia kulifanya.
 Kinana  alisema  kuwa  kuna  mitaa 150 katika  jimbo la Iringa mjini na mtaa mmoja pekee  wa Chadema  huku kata  zipo zaidi  ya 17 kata  moja ni ya Chadema  sasa  ni namna gani  CCM ishindwe  ubunge   jimbo hilo  hilo kama si tamaa za  uongozi  kwa baadhi ya  wagombea.
Hivyo  aliwataka   viongozi hao wa CCM kujaribu kusoma  alama za nyakati na  iwapo watajua  kuingia  wajifunze na kutoka kwani  kuna  wakati wa  kuchokwa  ni lazima  wakubali  kuondoka badala ya  kung’ang’ania  kugombea .
Pia  katibu   huyo aliwataka  wana CCM kujifunza  kujiuliza kwa  wananchi  wengine kama  wanakubalika ama  hawakubaliki badala ya  kusimamia  maamuzi yao ya  kuingia kugombea  bila  kupendwa  na  wananchi na kuwa kosa  lililofanyika mwaka 2010  kamwe  halitajirudia  tena.
“ Ni mambo ya  ovyo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya  CCM ndio ambayo yamekigharimu chama   na kuwa jimbo la  Iringa mjini  hakuna  mpinzani  ila wapo wanaotafuta  kusikilizwa  katika mambo yao na  iwapo CCM itatenda  mema kwa kusikiliza  wananchi  jimbo la Iringa mjini  hakuna  upinzani  ila  upuuzi ,rushwa ndani  ya CCM na  serikali  yake ndio  imekigharimu  chama   hicho “alisema 
Alisema kuwa  ndani ya  serikali   hii mwananchi anatafuta haki yake hapati  hadi atoe  rushwa  huku  viongozi  waliopo ndani ya CCM badala ya  kushughulika na mambo ya  wananchi wanashughulika na mambo yao  wenyewe  kwa ugomvi usio kwisha .
“ Tunapoteza majimbo na kata kwa  ajili ya  uroho  wa  uongozi kwa baadhi yetu na  kushindwa  kushuka kuwasikiliza  wananchi wa chini hali  inayozalisha malalamiko ya  wananchi na  kupelekea  kuhamia vyama  vya  upinzania”
Akihutubia huku  akishangiliwa na  umati mkubwa  uwanjani  hapo  Kinana  alisema  kuwa  amefika  jimbo la Iringa mjini  kuwaeleza mambo ya  kimaendeleo  sio  kumsema  mchungaji Msigwa  .
Hivyo  alisema  kuwa  iwapo  jimbo la Iringa mjini  litapata  mgombea  mgombea  mzuri  hakuna   upinzani  katika  jimbo  hilo ila  kama  ugomvi  wa madaraka  utaendelea  itakuwa ni kazi kupata  mgombea  wa  CCM .
Katibu  mkuu  huyo alieleza  kusikitishwa kwake na  ushuru mbali mbali   kwa wananchi wanaojitafutia maisha  yao huku  viongozi  wakijiweka mbinguni na  wananchi  wao.
Japo alisema  kuwa  kazi  zilizofanywa na CCM na serikali yake ni kubwa na kuwa hata  miradi ya  barabara  inayoendelea  kujengwa  ni jitihada za  serikali ya  CCM chini ya rais  Benjamin Mkapa  hivyo  mbunge hana sababu ya  kujisifu  kwa  kazi hizo.
“ Nawaambieni  wala  hamta nisikia  nikishughulika na kumzungumzia mbunge  wenu hapa  sina Time  mimi nashughulika na  mambo ya  wananchi kwani  mbunge  wenu ni klazi yake  kutukana kila mmoja na kuhamasisha maandamano yasiyo kwisha “

No comments:

Post a Comment