Na Imelda Mtema
MSANII
anayekuja kwa kasi anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’
amewaasa wasanii wenzake kujali afya zao kwa kupenda kupima ugonjwa wa
Ukimwi mara kwa mara.
Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo alisema kuwa kungekuwa na
taratibu kabisa za kupima ugonjwa huo si kwa nia mbaya ili kuweza
kujuana maana kwenye vikundi vya sanaa ndiko kwenye vitendo vingi viovu.
“Ni kitu kizuri sana tena kupima kwa hiari na hivyo vingeweza
kusaidia kuwaepusha wasanii wachanga wanaorubuniwa na viongozi wa
vikundi ili kupewa nafasi ya kuonekana kwenye runinga,” alisema Sabby.
No comments:
Post a Comment