Msumbiji:Serikali na Renamo waafikiana
25 Agosti, 2014
Habari kutoka Msumbiji zinasema
serikali ya nchi hiyo imetiliana saini na chama cha upinzani cha Renamo
ili kumaliza uhasama kuelekea uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Mkataba huo unafuatia unafuatia mapigano ya
chini kwa chini kati ya wafuasi wa Renamo wenye silaha na majeshi ya
serikali. Mwezi Oktoba mwaka jana Renamo walijitoa katika mkataba wa
amani uliotiwa saini kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, mkataba ambao
ulimaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Wiki iliyopita
ikiwa sehemu ya makubaliano, serikali ya Msumbiji ilianza kuwaachilia
wafungwa wa Renamo waliokuwa wamekamatwa katika mapigano ya hivi
karibuni.Tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake tarehe 25 Juni 1975 kutoka kwa wakoloni wa Kireno imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na waliokuwa waasi wa renamo na sasa ni chama cha siasa cha upinzani.
No comments:
Post a Comment