Wednesday 17 September 2014

KWELI::Petit Man Adhibitisha Kuwa Mdogo wa Diamond ni Mchumba Wake na Muda si Mrefu Watafunga Ndoa

Meneja wa msanii, Mirror na mfanyakazi wa kampuni ya Wema Sepetu, Endless Fame Films, Petit Man ambaye awali alidaiwa kuwa na uhusiano na Kajala, kisha kuwa na mdogo wake Vanessa Mdee, amethibitisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yake Diamond Platnumz, Esma na kwamba ana mipango ya kufunga naye ndoa.

“Ni kweli Esma ni mchumba wangu na Mungu akijalia soon tunafunga ndoa,” alisema Petit kwenye kipindi cha My Playlist cha Clouds TV. Alipoulizwa jinsi Diamond anavyouchukulia uhusiano wao, alisema: Unajua siwezi kumsea moyo wake lakini naona kawaida na hamna tatizo lolote.”

No comments:

Post a Comment