Tuesday 16 September 2014

SIASA::DK SLAA ATEULIWA TENA KUWA KATIBU MKUU WA CHADEMA


Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chadema,  Dk. Willbrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika kuwa na Salum Mwalim ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar. 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amewateua Dk. Willbrod Slaa kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Salum Mwalim ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar. Viongozi hao wameteuliwa jana usiku na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema hivyo kufikia tamati ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho.
Mhe. John Mnyika anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na kamati kuu ya chama hicho kwa kudaiwa kuvunja katiba ya chama.

No comments:

Post a Comment