Tuesday 16 September 2014

TATIZO LA WANAUME KUWAHI KUFIKA KILELENI (PRE MATURE EJACULATION)

WIKI iliyopita nilifungua somo muhimu sana kwa wanaume ambalo ni tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni au kuwahi kumaliza katika tendo la ndoa ikiambatana na uchovu wa ghafla wa kushindwa kurejea katika tendo na mbaya zaidi usingizi pia huwakumba ghafla wakiwaacha wenza wao bado na hisia kali za mapenzi.
Nilisema ninaliita hili kuwa ni janga la kitaifa kwa kuwa kliniki kwangu nimekuwa nikipokea wanaume wengi wenye tatizo hili lakini sababu ya pili ya kuliita janga la kitaifa ni kuwepo wanaume wengi wenye tatizo hili lakini hawajui kama ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine, lina vyanzo vyake na tiba kamili kwa hiyo wengi wao hubaki na tatizo hili likiwatafuna mpaka uzeeni.
Niliishia kwenye vyanzo na nilianza kwa kusema kwamba:
1. Kujichua (masturbation ) ni chanzo kikubwa cha tatizo hili kwa kuwa mara nyingi mtu mvulana anapoanza mchezo huu huwa anafanya kwa siri na huhitaji amalize mapema kabla hajakutwa na watu na tabia hii hujijenga kisaikolojia na kujikuta mvulana/mwanaume huyu huendelea na tatizo hili la kuwahi kumaliza hata katika tendo halisi.
Madhara haya ya kujichua huambatana na uume kusinyaa, kuwa mfupi na mwembamba tofauti na awali. Tafiti za kitabibu zinatabanaisha kwamba kila mwanaume aliyewahi kujichua mfululizo katika maisha yake ni lazima atakumbwa na tatizo hili kipindi fulani cha maisha yake.
2. Msongo wa mawazo. Wanaume wengi hasa wa mijini hujikuta katika msongo wa mawazo usiokwisha na hivyo hurudi nyumbani kutoka katika shughuli zao za kila siku.
3. Kukamia kupita kiasi.
4. Uoga/kutojiamini. Hali hii huwakumba wanaume wasio na taarifa kwamba wao ni wakamilifu, wanaume ambao hujidharau na kujiona hawafai kuwa na mwanamke wa hadhi fulani
5. Dr. Abrahams James wa Saint Magreth Clinic iliyopo Washington Dc katika andiko lake liitwalo `Sex and Fertility` la mwaka 2011,
amesisitiza kwamba wanaume kutofuatilia majarida /elimu au taarifa za mbinu mbalimbali za kumwezesha mwanaume kuchelewa kufika kileleni, huchangia kuendelea kwa tatizo hili kwa kizazi na kizazi na hasa kwa wanaume wa mijini ambao wengi wao miili yao haifanyishwi mazoezi kwa kazi zao au hata kwa kupanga muda.
Anasisitiza kwamba mwanaume anapopata ufahamu huu hupata hali ya kujiamini na hivyo kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa.
6. Ulaji mbovu ukiambatana na uzito kupita kiasi.Ulaji wa siku hizi hasa mijini ni mbovu kwa maana ya kwamba watu hujali rangi na ladha na si viini lishe vilivyomo na pia hawajali matokeo mabovu ya ulaji huo. Inashangaza kuona wasomi wengi na watu wenye uwezo kifedha wakiongoza kwa ulaji mbovu unaosababisha pamoja na mambo mengine, kukumbwa na tatizo la wanaume kuwahi kufikia mshindo na kutoweza kuendelea mpaka masaa mengi au hata siku zaidi ya moja zipite.
7. Kutofanya mazoezi na mwili kuwa legevu bila stamina ya kutosha. Inashangaza kuwaona watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi au wazee au wagonjwa ndio wapo mazoezini asubuhi na jioni.
Hiki ni kiashiria kwamba watu hufanya mazoezi pindi wanaposhauriwa na daktari kwamba hiyo ndiyo suluhu ya wao kuendelea kuishi ilhali mazoezi yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ili pamoja na faida zingine, yawasaidie wanaume kuchelewa kufika kileleni hasa wale ambao bado hawajakumbwa na tatizo hili.

No comments:

Post a Comment