SIKU
chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na
bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangusha bonge la sherehe
iliyofana ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo
jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao, Ijumaa lilikuwepo.Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
Akiwa kwenye sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo kuleta burudani nyingine.
Kwa upande wake, Rose alisema: “Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na leo naanza kurejesha furaha yangu na kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu, kwani siku chache zilizopita nilikuwa siko poa, ila leo nafurahi na ndugu na marafiki zangu kwenye siku yangu muhimu, najua pati hii imekuwa safi na hakuna aliyeboreka maana mambo yote yako vyema kabisa.”
No comments:
Post a Comment