Thursday, 18 September 2014

JIPU HILO::RAIS KUTOKUWA NA ‘MENO’ KWENYE BUNGE LA KATIBA ALAUMIWE NANI?

KWANZA kama ilivyo ada nimshukuru Mungu kwa kuniweka hai nikiwa na afya njema.
Wiki iliyopita nilieleza jinsi muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyozitesa serikali za muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nikasema kamati na tume nyingi ziliundwa na fedha za walipa kodi, nyingi zikatumika lakini mgogoro upo palepale.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Kuna walioshauri kuwa rais alivunje bunge lakini Mwanasheri Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akasema, hawezi kulivunja kwa sababu sheria haimruhusu, kwa maneno mengine hana meno ya kumaliza tatizo.
Lakini sasa imedhihirika kuwa hatima ya Bunge Maalum la Katiba imebaki mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, yuleyule aliyetajwa kuwa hana mamlaka ya kulivunja baada ya kuandikiwa barua na uongozi wa bunge hilo akitakiwa atoe ufafanuzi wa kisheria kuhusu tarehe ya mwisho ya kumaliza vikao vyake lakini pia alikutana na wapinzani wa serikali yake.
Ameandikiwa barua kutokana na muda uliopangwa kwenye ratiba ya bunge hilo kuzua utata wa kisheria na kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
Ratiba ya Bunge Maalum la Katiba inaonyesha kuwa limepanga kuhitimisha vikao vyake mwishoni mwa Oktoba, tofauti na tarehe iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete Julai 28, mwaka huu ambayo ilitangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la Agosti Mosi.
Tangazo la rais linaonyesha kuwa awamu ya pili ya Bunge Maalum ingeanza Agosti 5, 2014 na kumalizika Oktoba 4, lakini ratiba ya Bunge hilo inaonyesha kuwa litamalizika Oktoba 31, siku ambayo Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta anatakiwa akabidhi kwa rais Katiba inayopendekezwa.
Hadi tunapoandika makala haya serikali bado haijatoa tangazo lingine kwenye gazeti la serikali kuongeza muda hadi mwishoni mwa Oktoba kama alivyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Sitta wakati akitoa ufafanuzi wa siku 60 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, Agosti 5, mwaka huu.
Sitta alisema kwa kadiri ya tafsiri, siku za kazi ni Jumatatu hadi Ijumaa ambazo wajumbe wanapaswa kufanya kazi na kwamba Jumamosi na Jumapili siyo sehemu ya siku 60 zilizoongezwa na rais.
Kuna mchanganyiko mkubwa kwani Katibu wa Bunge Maalum, Yahya Khamis Hamad alisema  hawajapata maelekezo ya ziada kutoka serikalini ambako waliiandika barua ya kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alikiri ofisi yake kupokea barua kutoka Bunge Maalum ikiomba ufafanuzi ambao ungeliwezesha kuongeza siku kwa lengo la kukamilisha kazi ya kujadili na kuandika katiba inayopendekezwa na kwamba maombi yao bado yanafanyiwa kazi.
Utata wa kisheria
Licha ya ahadi iliyotolewa na Sitta ni dhahiri kwamba suala hilo lina utata wa kisheria kutokana na kauli iliyowahi kutolewa na Mwanasheria wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema wakati akitoa ufafanuzi wa maana ya siku 70 ambazo bunge lilikaa mara ya kwanza.
Baada ya kusoma hati ya rais ya kuitishwa kwa bunge hilo, Februari mwaka huu, Jaji Werema alisema siku 70 zilizotolewa kwa mujibu wa tangazo la serikali ni za kikalenda na siyo siku za kazi kwa sababu wajumbe wa Bunge Maalum siyo watumishi wa kuajiriwa.
Kauli ya Jaji Werema haijawahi kutenguliwa na Mahakama au yeye mwenyewe na kwa msingi huo, kwenda kinyume chake ni kuvunja Sheria ya Kazi na Majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268 ya 2005.
Mgogoro mwingine unaojitokeza ni ratiba za vikao vya Bunge la Muungano ambalo limepangwa kuanza Novemba 4, 2014 na Baraza la Wawakilishi ambalo limepangwa kukutana kuanzia Oktoba 22, mwaka huu.
Kwa kawaida, vikao vya Bunge hutanguliwa na wiki mbili za vikao vya kamati za kudumu na ikiwa ratiba itabaki kama ilivyo, basi vitaingiliana na vikao vya Bunge Maalum ambalo ratiba yake imepangwa kuendelea hadi Oktoba 31, mwaka huu.
Hakuna ambaye atabisha nikisema kuwa  kwa jinsi ratiba ya Bunge Maalum la Katiba ilivyopangwa lazima itaingilia shughuli za Bunge la Muungano na lile la Baraza la wawakilishi hivyo uamuzi unapaswa ufanywe ili kuepusha mgongano huo.
Njia pekee ni kumuomba Rais Kikwete asogeze mbele vikao vya mabunge mengine ili Bunge Maalum la Katiba lipate nafasi ya kuendelea na kikao japokuwa wapo walioona kuwa hana uwezo wa kulisitisha au kusogeza mbela vikao vyake.
Hakika masuala haya ni mazito na yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi haraka. Lakini wengi tunajiuliza, waliokuwa wakipanga vikao vya Bunge Maalum la Katiba walikuwa hawayajui hayo? Au ni kutaka kumchosha rais bure na kumsababishia atupiwe lawama?
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

MTABIRI ALITABIRIA PENZI LA RAY, CHUCHU

Na Gladness Mallya
MTABIRI maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein amelitabiria penzi la waigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans kuwa litakuwa na mafanikio makubwa kwani wanaendana.
Waigizaji wa filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans wakipozi.
Akizungumza na Amani, Hussein alisema kinyota Ray nyota yake ni aina ya Mashuke ambapo Chuchu nyota yake ni Mapacha ambazo zinaendana kwani wanashirikiana sayari moja ambayo ni Mercury na siku yao ya bahati ni Jumatano.
Mtabiri maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein akiwa ndani ya ofisi za Global.
“Japokuwa Ray amehangaika sana lakini kwa Chuchu amefika hivyo ajitahidi kutulia na asihangaike tena na wanawake kwani huyu wanaendana tofauti na wale wanaotajwa kuwa alikuwa na uhusiano nao yaani  Johari na Mainda,” alisema Hussein.

KUMBE BADO::UKWELI KUHUSU HABARI YA DIVA KUTAMKA ZITTO NI MUME WAKE

KATIKA Gazeti la Amani Toleo Namba 829 la Septemba 11-17, 2014, kulichapishwa habari ukurasa wa mbele iliyosomeka: “DIVA: ZITTO NI MUME WANGU.” Ikikolezwa na dondoo ‘Adai ni mke anayetambulika kisheria’ na ‘Asema hayuko tayari kuachana naye kirahisi,’ ambayo uongozi wa gazeti umekusudia kwa nia njema kutoa ukweli juu ya habari hiyo.
Loveness Malinzi (Diva).
Ufafanuzi huu unalenga kumaliza mkanganyiko uliojitokeza hasa baada ya kuwepo kwa madai kutoka kwa mhusika ambaye ni Loveness Malinzi (Diva) kuwa, hakuzungumza na gazeti kile kilichoandikwa na kwamba alikuwa anazushiwa; madai haya aliyawasilisha chumba cha habari kwa njia ya simu na sehemu kuyaweka kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.
Kama hilo halitoshi, Diva alikana kuzungumza na mwandishi wa habari hiyo  ambapo alisema mazungumzo yao yalihusu mwaliko wa Kipindi cha Global TV Online ambacho kinarushwa na mtandao unaoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers inayomiliki pia Gazeti la Amani na si vinginevyo.
Malalamiko haya ya Diva yalikuja muda mchache baada ya gazeti kutoka likiwa na habari hiyo ambapo jopo la wahariri wa Amani kabla ya kuchapisha habari hiyo walijiaminisha kuwa ni ya kweli kutokana na taarifa pamoja na vielelezo vya rekodi ya sauti ya mazungumzo alivyoviwasilisha mwandishi kwenye dawati kuthibitisha kuwa alifanya mazungumzo na mhusika kuhusiana na msingi wa habari nzima iliyoandikwa.
Mheshimiwa Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini.  
Kama tulivyoeleza, baada ya habari hiyo kutoka na kipande cha sauti kuingizwa  kwenye Tovuti ya Global Publishers, ndipo yalipoibuka madai hayo huku baadhi ya wasomaji wakieleza kuwa ile siyo sauti ya Diva; hapo ndipo uongozi wa gazeti ulipoamua kufuatilia ukweli na kubaini yafuatayo.
Pamoja na ukweli kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini) na Diva wana ukaribu, mazungumzo kati ya mwandishi na mwanadada huyo kuhusiana na kauli yake ya: “Zitto ni Mume Wangu,” hayakufanyika na kwamba mwandishi alipika habari na kutengeneza sauti ya Diva kwa lengo la kuwahadaa wahariri kwa nia mbaya!
Kwa msingi huo sisi kama chombo cha habari makini, kinachosimamia weledi, kulinda na kuheshimu haki za binadamu; tunachukuwa nafasi hii kumuomba radhi Diva, Mheshimiwa Zitto, sanjari na jamii kwa ujumla kwa usumbufu wowote uliosababishwa na habari hiyo.
Aidha, uongozi unapenda kuutangazia umma kuwa, hatua kali za kinidhamu zimeshachukuliwa dhidi ya mwandishi husika sambamba na onyo kwa viongozi wote wa gazeti kwa udhaifu uliojitokeza katika habari hiyo.
Tunaomba jamii ielewe kwamba Global Publishers siku zote inasimamia UKWELI na kamwe hairuhusu kabisa habari za uongo kuandikwa katika magazeti yake.
Jamii iendelee kutuamini na kushirikiana nasi katika kusimamia weledi wa uandishi wa habari. Milango ya kukosolewa iko wazi, hivyo kwa mwenye malalamiko yoyote juu ya habari zetu, iwe ni uongo au kutotendewa haki, asisite kuwasiliana na viongozi kwa hatua zaidi. Ndimi, Mhariri Kiongozi, Magazeti Pendwa.

UMOJA WA VIJANA WAZALENDO WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DAR ES SALAAM WATOA TAMKO LA KULAANI KAULI ZA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KWA MADAI YA KUHAMASISHA MAANDAMANO

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Omary, akisoma tamko hilo, Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Omary (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akisoma tamko hilo. Kulia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata na Mwanachuo Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Rehema Akukweti.

Wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.


Mwanachuo wa UDSM, Gulatone Masiga akijibu maswali ya waandishi wa habari. Kushoto ni Mwanachuo Mwita Nyarukururu na Mwenyekiti wa umoja huo, Mussa Omary.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata, akichangia jambo wakati wa kujibu maswali ya wanahabari.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanachuo Mussa Mashamba kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya wanahabari. Kulia Massoro Kivuga na William Haule. 

Dotto Mwaibale

UMOJA wa Vijana Wazalendo wa Vyuo Vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam, wamemshukia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe kwa kutaka kuitisha maandamano ya kupinga Bunge Maalum la Katiba.

''Sisi umoja wa vijana wa vyuo vikuu tunapinga vikali kauli hiyo na kulaani vikali ya kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano,''alisema.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa vijana hao Mussa Omary alisema kauli aliyotoa mwenyekiti huyo inahamasisha kuleta mgogoro nchini.

''Tumesononeshwa na kauli hiyo ya kibabe ya kiongozi huyu ya kuhamasisha vurugu ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha vita,''alisema.

''Tulimsikia akiahidi maandamano bila kikomo kwa kibali cha polisi au hata bila kibali cha polisi mbele ya wajumbe ambao wengine sio watanzania,''

Omari alisema uzito wa jambo hilo unaonesha wazi kuwa Mwenyekiti huyo hasatahili hata kidogo kuweza kupewa uongozi wa nchi hii.

Aliongeza kuwa mwenykiti huyo na viongozi wenzakae wanatumia maandamano na damu za watanzania kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao hawaitakii nchi hii mema.

''Wakiandaa maandamano haya huwa wanapiga picha na kuwatumia wafadhili wao na kupata fedha na kujenga majumba na kununua magari makubwa na huku watanzania wakiendela kuathirika,''alisema.

Alisema thamani ya mtanzania mmoja ni kubwa kuliko hiyo katiba mpya wanayodai ni vizuri watanzania kuacha kuwaunga mkono na kufanywa kama mbuzi wa kafara.

Aliongeza kuwa ni vyema vyombo vya dola visiweze kuvumilia kauli hiyo iliyotolewa hivyo kuendelea,kulinda kutunza na kuweza kuiendeleza amani ya nchi.

''Ni vizuri watanzania wakakaa na kufikiria kauli hii ya mwenykiti huyu na kujiuliza kuwa je ni kweli anaweza kuwa kiongozi wa nchi hii,''alisema.

Naye,mmoja wa wanafunzi hao Theodera Nalaya alisema ni vizuri tukaliachia bunge maaluma likafanya kazi yake ya kutafuta katiba mpya.

''Sisi kama vijana wa vyuo vikuu msimamo wetu ni kuwa tuliachie bunge la katiba likafanya kazi yake na muda ukifika wa kutoa maoni yetu ukifika tutatoa maoni yetu na si kuvamia,''alisema.

MAMIA WAMSINDIKIZA MBOWE POLISI


MAMIA ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), asubuhi hii wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kuelekea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Mbowe amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Katika tukio hilo, baadhi ya waandishi wa habari wamekimbizwa na polisi waliokuwa na mbwa wakitakiwa kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika makao makuu hayo ya polisi.

Jamani Mke wa Rafiki Yangu Anadai Nimuongezee Njia ili Wakati wa Kujifungua Asipate Shida..Ushauri


Jamani Udaku Specially Mwenzenu naingia katika vishawishi kutoka kwa mke wa rafiki yangu kabisa, ni hivi rafiki yangu kasafiri kikazi nje ya nchi kwa muda sasa, huku nyuma amemuacha mke wake ambae ana ujauzito wa miezi nane sasa bado mmoja ajifungue , sasa juzi nimekutana nae tukapata lunch pamoja sehemu, basi katika kuongea ongea akaniambia dokta wake amemwambia kipindi hichi inafaa ampe sana yale mambo mumewe ili njia ifunguke asipate shida wakati wa kujifungua , sasa mume wake ndo hayupo katika kutaniana taniana akaniambia kama sita jali na nitakuwa msiri niwe nampa kitu mpaka atakapojifungua ili kuongeza njia...Bado sijamjibu na leo nimekuta message akikumbushia Jambo Hilo ..Wadau Nifanyaje?

HII NDIO HOTEL ILIYOJENGWA MIAKA 134 ILIYOPITA KATIKATI YA MAJI HUKO UINGEREZA.INAITWA SPITBANK FORT

HOTELI ya Spitbank Fort ikionekana kwa juu ikiwa imejengwa mwaka 
1879 katikati ya kina maji ya habari nchini Uingereza  ikiwa na umri wa miaka 134.

Hapa ikionekana katikati ya kina cha maji ya bahari. 
Sehemu ya mbela ya hoteli hiyo. 


Ndani 
Sehemu ya kupunga upepo 
mandhali ya ndani. 
hii nayo ni sehemu nyingine ya kupunga upepo 
jiko 



hapa ni chumbani 


Mandhali wakati wa jiono muonekano wake.

Cheki Hapa Jinsi Mwigizaji Nora Alivyomchana Live Live Kajala Masanja


MWIGIZAJI kiwango enzi hizo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ aliyepotea kwa muda, ameibukia kwenye Runinga ya EATV na kumbutua staa wa mwenzake, Kajala Masanja kwamba, anatumia nafasi ya kuonekana kwenye filamu kujipatia wanaume kama si mabwana!

Akizungumza kupitia Kipindi cha Mkasi kinachoratibiwa na Mtangazaji Salama Jabir, Jumatatu iliyopita, Nora alisema fani ya uigizaji imevamiwa kwa sasa kwani kuna watu ambao wanaingia kwenye gemu ili wauze sura na kuonekana na wanaume wapate ‘soko’ kiulaini.

Aliongeza kuwa, watu hao kupitia vitendo hivyo wamekuwa wakiichafua tasnia kiasi cha wote kuonekana hawafai (samaki mmoja akioza, ni wote).

Nora alikwenda mbali zaidi alipoulizwa na Salama ni nani na nani hawafai na nani wanafaa, alishindwa kuwataja kwa majina moja kwa moja lakini mtangazaji huyo akaomba ataje majina yeye kisha Nora aseme kama anafaa au hafai!
Salama: “Kajala.”

Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Batuli.”
Nora: “Huyo pia hamna kitu.”
Salama: “Lulu.”
Nora: ”Huyo safi.”

Salama: “Mlela (Yusuf).”
Nora: “Huyo hamna kitu.”
Salama: “Steve Nyerere.”
Nora: “Huyo hamna kitu.”

Salama: “Hemed (Suleiman).”
Nora: “Hamna kitu hapo.”
Juzi gazeti hili lilimsaka Kajala kwa njia ya simu hakupatikana, lakini mmoja wa watu wake wa karibu alisema staa huyo ameshangaa sana Nora kutaka kurudi juu kwa kutumia jina lake.

“Kajala amezima simu, lakini kamshangaa sana Nora, alishazimika, sasa anaonekana anataka kuwaka tena kwa kutumia jina lake,” alisema mpambe huyo.
GPL

Picha 5 za kilichotokea kwenye mpaka wa Sudan na Uganda



Uganda 5
Ripota wa TZA nchini Uganda Bill the African ameripoti kuhusu hii ya vurugu kubwa kutokea kwenye mpaka wa Uganda na Sudan eneo la Ufoju kutokana na raia wa nchi hizi mbili kutoafikiana kwenye baadhi ya mambo ambapo pia baadhi ya viongozi wa Uganda kwenye eneo hilo walikamatwa na Polisi wa Sudan.
Kikubwa kinachosababisha vurugu hizi ni mipaka ya hizi nchi kushindwa kujulikana kila mmoja anatakiwa kuishia wapi ambapo pia Waganda ambao wamekua wakiingia Sudan wamekua wakikamatwa na Polisi wa Sudan na kupewa mateso makubwa.
Uganda 4
Jeshi la Polisi Uganda limesema kwamba katika vurugu hizi karibu nyumba 15 za raia wa Sudan wanaoishi Uganda zimechomwa moto likiwemo kanisa la kipentekoste linalodaiwa kuwa la raia wa Sudan.
Uganda 3
Uganda 1
Uganda 2

HUYU NDIYO MTOTO WA MAAJABU MTANZANIA MWENYE UWEZO WAKUONGEA NA WANYAMA



MTOTO Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alizua kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo kimaajabu.

Mtoto Happiness (10) anayedaiwa kuzua kizazaa mjini Zanzibar.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye Happiness alianza kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye uwanja wa ndege kisiwani humo wiki iliyopita.
Alisema maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.
Kwa mujibu wa mama huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo.
Zefania alisema wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja alijitokeza na kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.

Mtoto Happiness akiwa na mama yake mzazi, Sarah Zefania.
“Akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.
“Baada ya kushuhudia vituko hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii ambako nako wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na kuwaambia kuwa angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu ya paa na kutaka kutoka.
“Yaani kwa muda mfupi waliokaa naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema amewahenyesha vya kutosha ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi nikaenda kumfuata,” alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua bandarini Dar.
 

Mtoto Happiness katika pozi.
Paparazi wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama Happiness.
Akizungumzia historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana mawasilino mazuri.
Mama huyo alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake

Wednesday, 17 September 2014

Le Mutuz Amuonyesha Baby Wake na Kumwagia Sifa Kedekede 'Nampenda Mpaka Nasinzia'



Udaku Specially Imefanikiwa kupata Picha ya Baby ake Lemutuz , leo kupitia Instagram  yake @lemutuz_nation Mzee Mzima na Business Man wa Ukweli Lemtuz Amepost Picha Hiyo Hapo Juu na Kuandika Maneno haya Hapa Chini:

Wanaume Wanaowatelekeza Watoto Wao Nchini Kenya Wanakiona Cha Moto Kupitia Facebook

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri, Huu Ndio mtandao ulio Weka Wazi Kuwa Prezzo hatoi matunzo kwa Mtoto wake hivi karibuni

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf

Wanaume Wanaowatelekeza Watoto Wao Nchini Kenya Wanakiona Cha Moto Kupitia Facebook

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri, Huu Ndio mtandao ulio Weka Wazi Kuwa Prezzo hatoi matunzo kwa Mtoto wake hivi karibuni

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf

Wanaume Wanaowatelekeza Watoto Wao Nchini Kenya Wanakiona Cha Moto Kupitia Facebook

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri, Huu Ndio mtandao ulio Weka Wazi Kuwa Prezzo hatoi matunzo kwa Mtoto wake hivi karibuni

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf

Wanaume Wanaowatelekeza Watoto Wao Nchini Kenya Wanakiona Cha Moto Kupitia Facebook

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri, Huu Ndio mtandao ulio Weka Wazi Kuwa Prezzo hatoi matunzo kwa Mtoto wake hivi karibuni

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf

Wanaume Wanaowatelekeza Watoto Wao Nchini Kenya Wanakiona Cha Moto Kupitia Facebook

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri, Huu Ndio mtandao ulio Weka Wazi Kuwa Prezzo hatoi matunzo kwa Mtoto wake hivi karibuni

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf