Thursday, 9 October 2014

INATAKA UJASIRI::SABBY: WASANII TUPIME HIV

Na Imelda Mtema
MSANII anayekuja kwa kasi anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amewaasa wasanii wenzake kujali afya zao kwa kupenda kupima ugonjwa wa Ukimwi mara kwa mara.
Msanii anayekuja kwa kasi anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’.
Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo alisema kuwa kungekuwa na taratibu kabisa za kupima ugonjwa huo si kwa nia mbaya ili kuweza kujuana maana kwenye vikundi vya sanaa ndiko kwenye vitendo vingi viovu.
“Ni kitu kizuri sana tena kupima kwa hiari na  hivyo vingeweza kusaidia kuwaepusha wasanii wachanga wanaorubuniwa na viongozi wa vikundi ili kupewa nafasi ya kuonekana kwenye runinga,” alisema Sabby.

HABARI NA PICHA:::KASEMA NI LAZIMA

KIJIJINI::WANAKIJIJI WACHEZA MUZIKI KUSHANGILIA UMEME

WAKAZI wa kijiji cha Mbegasera wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, wameshindwa kuzuia furaha yao na kuamua kusakata muziki baada ya umeme kufika kijijini hapo na wananchi kuunganishwa kwenye nyumba zao, ambazo walilazimika kuezua sehemu ya nyasi na kuezeka kwa bati ili kufungiwa nishati hiyo. 
 
Hayo yalionekana hivi karibuni wakati Watendaji wakuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), walipotembelea maeneo mbalimbali nchini kuangalia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini wanayosimamia.
Msafara wa REA ulipopita kwenye kijiji hicho, ulishuhudia moja ya nyumba iliyoezekwa kwa nyasi na kuezuliwa sehemu kidogo na kisha kuezekwa kwa bati, ikiwa imeunganishwa umeme na unawaka, hivyo kuwafanya wanakijiji hao kuserebuka kwa kucheza.
"Tunacheza sisi tuna furaha ya umeme, hatukuwahi kuuona hapa kwetu, hadi uende mjini ndio kuna umeme, lakini sasa tunao acha tusarebuke, wala hatuleti ugomvi na mtu hapa", alisema Zanisha Kawaya mkazi wa eneo hilo.
Alisema wakati mradi huo unaanza kutekelezwa kijijini hapo, wananchi waliambiwa umuhimu wake na kuhamasishwa kujiandikisha kwa wale wanaotaka kufungiwa umeme, kwa kutoa shilingi 27,000 na mradi ulipokamilika walipata umeme.
Awali Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa REA, Bengiel Msofe alisema hadi sasa wananchi 248 wa vijiji vinne vya wilaya ya Kilosa wameunganishiwa umeme kupitia mradi wa nishati vijijini, unaotekelezwa na wakala huyo.
Alisema lengo la kuwaunganisha wateja 300 wa vijiji hivyo vinne ambavyo ni Kisanga, Mbegasera, Msolwa na Kibaoni ambavyo wateja hao 300, wanaunganishiwa nishati hiyo kwa gharama ya bei ya ruzuku ya shilingi 27,000 tu badala ya ile ya kawaidia ya Sh 139,000.

UDAKU::LUCY KOMBA: NIMEISHI NA MR. WIKI MBILI TU!

NaGladness Mallya
MSANII mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba amefunguka kwamba baada ya kufunga ndoa  hivi karibuni ameishi na mumewe Janus kwa wiki mbili tu.
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba akiwa na mume wake mumewe Janus.
Akizungumza na paparazi wetu, Lucy alisema kwa sasa amebaki Bongo peke yake ikiwa ni baada ya mumewe kwenda kwao Denmark ambapo alitakiwa kurudi kazini lakini bado anafanya maandalizi ili amfuate.
“Mume wangu alikaa kwa wiki mbili tu baada ya kufunga ndoa nikamwambia aniache ili nimalizie kufanya maandalizi ya kumfuata huko kwao Denmark ambapo mpaka sasa sijajua nitaenda lini maana bado sijamaliza mambo yangu ila tunaaminiana na tumeshazoea kwani tangu wakati wa uchumba tulikuwa tuko mbalimbali lakini nitaenda.
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba akipozi.
“Nikienda huko nitakaa kwa miezi mitatu nitarudi hapa Bongo kusalimia na kukaa kama wiki kadhaa, nampenda sana mume wangu na ninammis kwa kweli,” alisema Lucy Komba.

TAFAKURI YA LEO:::CCM WALIKUJA KUSOMA HAPA..JE,WALITOKA??

magamba         
 Kibao Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Nsimbo

SOKA LONDON::MACHO YA PANZI>>PIGO ARSENAL, OZIL NJE HADI 2015 BAADA YA KUUMIA GOTI

KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake, Mesut Ozil kuumia na anatakiwa nje kwa kipidi chote kilichobaki kumaliza mwaka 2014.
Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo vya MRI katika goti lake na Chama cha Soka Ujerumani kimethibitisha atakuwa nje kwa miezi mitatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hakufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Ujerumani mjini Frankfurt baada ya kuanza kulalamika juu ya hali yake.
Mesut Ozil atakuwa nje kwa kipindi chote kilichobaki mwaka 2014 baada ya Chama cha Soka Ujerumani kuthibitisha kuumia kwake goti

Ozil hajaonyesha dalili kubwa za maumivu katika miezi ya karibuni na amecheza mechi tisa msimu huu, akifunga bao moja.
Taarifa ya Arsenal imesema: "Ozil alilalamika kuwa na maumivu ya goti la kushoto baada ya mechi na klabu ikakishauri Chama cha Soka Ujerumani kumfanyia uchunguzi atakapojiunga na kikosi cha timu ya taifa.
"Klabu itamfanyia uchunguzi wa kina na ni mapema sana kusema Ozil atakuwa nje kwa muda mrefu kiasi gani".
Ozil, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mwaka jana, amekuwa akikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango akiwa na jezi ya Arsenal. 
Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi wa pili ndani ya msimu mpya, ni pigo kwa kochaa Arsene Wenger ambaye sasa idadi ya majeruhi inaongezeka katika timu yake, Ozil akkungana na Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud pamoja na Mikel Arteta.

ELIMU YA MAHABA::NANI NA NINI KINATANGULIA KATIKA UHUSIANO?

MAISHA ya kimapenzi, hasa katika nchi masikini kama Tanzania, yamebadili uelekeo na kuonekana kama ni kitu kinachotanguliza masilahi badala ya upendo kama ilivyokuwa enzi za mababu zetu.
Enjo, kama alivyojitambulisha kwangu hivi karibuni, anasimulia kisa cha kusisimua.
“Nilikutana naye kwenye daladala, baada ya kunisalimia tukapiga stori hadi alipokaribia kushuka katika kituo chake, akaniomba namba ya simu. Kwa kuwa tulikuwa tumeshazoeana kidogo sikuona taabu, nikampa.
“Aliposhuka tukaendelea kuwasiliana kwa kutumiana sms, kwanza ilikuwa ni maneno ya kawaida tu, lakini baadaye akabadili na kuanza kunitongoza. Sikukataa wala kukubali, kwa sababu mtu mwenyewe nilikuwa simjui.
“Kwa muda kama wa siku mbili hivi tuliendelea kuwasiliana na hatimaye nikaona acha tu nimkubali. Basi alifurahi sana. Akataka siku tuonane nikamwambia sawa, tukapanga siku. Kama mara mbili hivi nilimuomba vocha na alishanirushia ya shilingi elfu tanotano.
“Siku ya ahadi nikamwambia anitumie nauli, akatuma shilingi elfu kumi, nikaenda sehemu tukakutana. Tukapiga stori sana, tukanywa, tukala, lakini akanishangaza eti siku hiyohiyo anataka tukafanye mapenzi. Yaani mtu tumekutana tu leo, hapana, nikamwambia siku nyingine, basi akalalamika sana na tulipoachana, hakunitafuta tena.”
Simulizi yake iliishia hapo, akaingia Innocent, kijana wa kisasa:
“Nilimuona facebook, nikamuomba urafiki akakubali, tukawa tunachat, kwanza ilikuwa kawaida lakini baadaye nikamchomekea, akakubali. Basi tukapeana namba za simu na mawasiliano yakaendelea.
“Siku ya pili tu akaniomba vocha, nikamwambia aache haraka, mambo mazuri hayataki haraka. Akasema eti alihitaji kuwasiliana na mama yake aliye mkoani, nikamwambia atafute maarifa mengine, mimi nafikiria namna ya kumfanyia mambo makubwa zaidi, hayo madogomadogo kama vocha yatatue mwenyewe.
“Akaniambia eti kama nashindwa vitu vidogo kama vocha, hivyo vikubwa nitaviweza wapi, nikamwambia subiri utaona. Basi spidi ya mawasiliano ikapungua, nikimpigia na kumwuliza kwa nini hatumi sms kama zamani, akaniambia simu yake haina salio.
“Basi na mimi nikanyamaza, baada ya siku mbili tatu nikampigia na kumwomba tuonane, akasema kama nitamtumia nauli atakuja, nikamwambia dada mbona unakompleini vitu vidogovidogo, kama vipi kopa kwa mtu uje nitakurudishia, akakataa, nikamwambia kama hana nauli basi apotezee. Nikaachana naye.”
Hizi ni simulizi mbili zenye ujumbe tofauti, lakini zinazowahusu vijana katika mahitaji yao ya kimapenzi. Wasichana wote wawili wanaonekana kufanana mahitaji, tofauti na wavulana.
Mvulana wa kwanza alijitahidi kutimiza mahitaji ya mwenza wake akiamini siku ikifika naye atapewa anachostahili. Lakini yule wa pili hakuweza kutoa mahitaji ya mwenza wake kwa wakati.
Maisha ya kisasa yameifanya dunia ya kimapenzi kubadilika sana. Wapo baadhi ya wasichana wanaoamini mwanaume anayewapenda, lazima ataonyesha kuwajali kwa kuwapa fedha na mahitaji yao mengine hata kabla hawajakutana kimapenzi.
“Mwanaume gani anashindwa kukutumia hata vocha, mtu anashindwa kukutimizia mahitaji yako sasa hivi ndiyo ataweza baadaye?” Hili ni swali unaloweza kukutana nalo kutoka kwa wasichana wengi, wanapozungumza kuhusu mwanaume wanayemhitaji.
Lakini pia baadhi ya wanaume wamekuwa wagumu kutimiza mara moja mahitaji ya wasichana. “Yaani hata hajanielewa vizuri, ashaanza kuleta matatizo yake, kwani kabla hajakutana na mimi vocha alikuwa anapata wapi. Nimtumie nauli? Kwani si anakuja kwa mpenzi wake anashindwa kujilipia elfu moja?”
Haya pia ni maswali unayoweza kukutana nayo kutoka kwa baadhi ya wavulana wanapozungumza juu ya tabia ya wasichana wanaotanguliza mizinga.
Kuna jambo tunalopaswa kuliangalia vizuri na ikibidi kujifunza, kitu gani kinatakiwa kutangulia wakati wa uhusiano katika hatua zake za mwanzo?
Mifano hiyo miwili hapo juu inaweza kuwa mwongozo mzuri kukupeleka kwenye aina ya uhusiano uupendao. Lakini kwa wasichana, ni vyema sana kuepuka kutanguliza mahitaji yako yanayohusu fedha, kwani wakati mwingine wanaweza kujikosesha bahati ya kumpata mtu mwenye malengo ya maisha kwa vile atamuona ni mtu mwenye kujali pesa badala ya upendo.

SAUDIA::Shabiki mwanamke awakera wanaume Saudia

Wanawake wa Saudi Arabia hawaruhusiwi kuingia uwanjani kushabikia mechi za soka
Shabiki mwanamke aliyekuwa akiishabikia timu ya soka ya Saudia katika eneo la milki za kiarabu amewakasirisha wanaume wengi katika mtandao wa kijamii nchini humo.
Kanda ya video iliyowekwa katika mtandao wa You tube ikionyesha alivyokasirishwa baada ya mchezaji wa Saudia kuchezewa rafu, imetizamwa na watu 400,000 na kupata maoni 1000.
Wengi waliotoa maoni yao ni wanaume waliokasirishwa na hatua ya mwanamke huyo kuwa ndani ya uwanja uliojaa maelfu ya wanaume.
Timu yake ilishindwa ndio maana akakasirika.
Nchini Saudi Arabia,wanawake wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi za soka,lakini kwa kuwa mechi hiyo ilikuwa ikichezwa katika miliki za kiarabu,shabiki huyo pamoja na wanawake kadhaa waliokuwa wakiishabikia Saudi Arabia waliweza kujiunga na mashabiki wengine wa kiume katika uwanja huo.

DSM::UPENDO>>UWT YATOA MISAADA MSIMBAZI CENTER JIJINI DAR

JAMANI WATANZANIA TUNAWEZAJI KUTUPA WATOTO KAMA HAWA? INANIUMA SANA
MISAADA YATOLEWA MSIMBAZI CENTER NA UWT ILALA NA MWENYEKITI NORA MZERU
MWENYEKITI UWT ILALA NORA MZERU AKIKABIDHI MSAADA MSIMBAZI CENTER JIJINI DAR
 AKISAINI KITABU CHA WANGENI
 
 

HATARI::TRAFIKI WA PICHA YA MAHABA WATIMULIWA KAZI

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioachishwa kazi.
ASKARI wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliopiga picha ya mahaba wakibusiana huku wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi na picha yao ikasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii wamefukuzwa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe amethibitisha leo kwa waandishi wa habari mkoani humo kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.

MAHABA NIUE::DIAMOND ATESEKA NA PENZI LA WEMA!

Stori: Richard Bukos
Imebumburuka kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ kumbe anateseka na penzi la mwandani wake, Beautiful Onyinye Wema Isaac Sepetu, Amani lina mkanda kamili.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ akwa ameshika gauni la mpenzi wake.
YATOKANAYO
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa, Diamond amekuwa akiumia na kuvumilia anapoitwa majina mabaya huku akisemekana hamuwezi Wema hivyo awaachie mapedeshee wenye ‘kisu’ kirefu.
“Hivi unajua kwa nini Diamond alimpa Wema zawadi ya Nissan Murano (gari)? Alijua asipofanya hivyo kuna mtu atafanya  na kweli ndivyo ilivyotokea kwa lile Gari BMW.“Nawahakikishieni kwa Chibu au Dangote (Diamond) alichezwa na machale,” kilidai chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao.
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI YA DIAMOND
Sasa ndani ya pati ya bethidei ya Diamond kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, kidume huyo alinaswa akiwa ameshikilia gauni la Wema kwa muda mrefu ili kuhakikisha haliburuzi chini kwa urefu.
Akimshikia gauni la mpenzi wake huku wakiingia ukumbini.
Wakati wa kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya BMW X6 alilopewa na menejimenti yake, ndipo kulipokuwa na sarakasi kubwa kati ya mastaa hao.
DIAMOND AHANGAIKA
Baada ya wageni waalikwa kutangaziwa kuwa kuna zawadi maalum ya jamaa huyo, watu waliombwa kutoka nje kuelekea eneo la maegesho ya magari (parking) ili kushuhudia makabidhiano hayo.
Hapo ndipo Diamond alipojikuta akihangaika zaidi na gauni refu la Wema akilishikilia na mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshika glasi ya ‘waini’ nyekundu.
Wakati wakitembea mdogomdogo kama maharusi, Diamond alijikuta akiwa kama mpambe wa bibi harusi kwa kumzunguka Wema mara kwa mara akilishikilia gauni hilo, shukurani ziende kwa mbunifu wake maana mtoto wa kike alitokelezea mashalaah!
Diamond akimuweka sawa mpenzi wake.
UPAJA WA WEMA NJE
Kuna wakati Diamond alilinyanyua gauni hilo na kusababisha ule upaja mweupe wa Wema kuwa nje huku midume ikiutolea udenda na wengine wakihisi jamaa huyo alifanya makusudi ‘kuwaringishia’.
“Ebwana Chibu mbona anamfunua Madam upaja unaonekana? Au anaturingishia ili tujue anakaa pazuri?” alisikika mmoja wa wanaume hao bila kufafanua kukaa pazuri alimaanisha nini.
WEMA ACHEKELEA, ATEMBEA POLEPOLE
Wakati Diamond akihangaika na gauni hilo, Wema alikuwa akichekelea kwa kuonesha uso wa tabasamu na kutembea polepole ili kumhenyesha staa huyo na kuthibisha kwamba kweli yeye ni Madam na kwamba Diamond anajua ‘kukea’.
Wema na Diamond wakifanya yao.
KIJASHO CHEMBAMBA CHAMTOKA DIAMOND
Hadi wanafika kwenye zawadi hiyo ya gari, kijasho chembamba kilimtoka Diamond ambaye alipokea ufunguo kwa mkono mmoja baada ya kuomba ashikiwe glasi ya ‘waini’ huku mkono mwingine ukiendelea kushikilia gauni hilo hadi alipomfungulia Wema mlango akaingia, naye akazunguka upande wa dereva.
Baada ya kulitesti gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 90, wawili hao walirejea ukumbini kwa staili ileile ya Diamond kuhangaishwa na gauni hilo hadi walipoketi meza kuu na kuendelea na ratiba.
NI ‘KAMZIZI’?
Kwa mujibu wa watu wapenda ‘ubuyu’ waliokuwemo ukumbini humo walisikika wakisema si bure, Diamond kuhangaika na Wema kiasi hicho hivyo huenda kawekewa ‘kamzizi’.
“Mimi nakwambia hata kama ni kumpenda kiasi gani lakini hii ni zaidi ya mahaba niue au kawekewa kamzizi, si bure kwa wanaume wa kizazi hiki kukea kiasi hiki,” alisikika mmoja wa wanawake waliokuwa wakimuonea wivu Wema na kumpa pole Diamond kwa kuhenya.

MBEYA::HONGERA JIJI KWA KUSIKIA KILIO CHA MTAA WA SOUTH STREET TUMEONA MMEANZA KUCHUKUA HATUA


Hatimae jiji la Mbeya limeanza kutengeneza barabara ya  South Street mtaa huu ulikuwa maarufu sana hapo nyuma na ulijulikana kwa jina la mtaa wa RTC  sasa unaitwa mtaa wa tunakopesha 
Hakika kazi tunaiona hivyo tunawaomba jiji mikamilishe mapema kazi hii ili muendelee na maeneo mengine ya jiji hili letu 
Hizi picha kabla barabara hii haijaanza kutengenezwa

Picha na Mbeya yetu

AFRIKA MASHARIKI::Gharama ya kupiga simu kupunguzwa

kupiga simu
Watuamiaji wa simu za mkononi nchini Kenya,Rwanda na Uganda hivi karibuni watakuwa wakipiga simu kwa bei nafuu,baada ya wahudumu wa simu kukubaliana kupunguza ada ya kupiga simu katika eneo lolote la Afrika Mashariki.
Ada ya kupiga simu katika nchi nyengine za Afrika mashariki zitapungua kwa asilimia 60.
Waziri wa mawasiliano nchini Kenya amesema kuwa watumiaji wa simu za mkononi watalipa ada za chini ili kupiga simu katika mtandao wowote katika taifa la Afrika ya Mashariki.
Wale walio katika mataifa hayo hawatalipishwa kwa kupokea simu.
''Tumepunguza ada ya kupiga simu katika eneo la Afrika Mashariki'',alisema waziri Fred Matiangi.
Kenya Rwanda na Uganda ni mataifa matatu kati ya matano ambayo yanaleta pamoja jumuiya ya Afrika Mashariki,inayolenga kupunguza vikwazo vya kibiashara .
Inatarajiwa kwamba wanachama wengine wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Burundi pia watatekeleza mpango huo,ili kuwashinikiza wahudumu wa simu katika mataifa hayo mawili kupunguza ada ya wateja wao kupiga simu wanapokuwa katika mataifa mengine ya afrika mashariki.
Nebert Rugadya ambaye ni mchambuzi wa maswala ya kiuchumi nchini Uganda ameiambia BBC kwamba ada ya kupiga simu kutoka mataifa mengine ya afrika mashariki ni ya juu mno.
''Kupiga simu nchini Kenya kutoka Uganda imekuwa ikigharimu shilingi 2000,lakini iwapo ada ya kupidga simu katika taifa lolote la Afrika Mashariki itapunguzwa basi simu hiyo itagharimu shilingi 260'',alisema Rugadya.
Hatua hiyo itapunguza gharama ya mawasiliano katika eneo hili mbali na gharama ya biashara.

ARUSHA::PEOPLE'S POWER>>TASWIRA ZA MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA JANA


Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, akihutubia katika mkutano uliofanyika jana kwenye Uwanja vya Samunge, Kilombero jijini Arusha.
Makamanda wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.
Umati wa wakazi wa Arusha waliohudhuria mkutano huo jana.

IRINGA::MOTO UMEWAKA NA KUUNGUZA NYUMBA MAENEO YA UHINDINI,MANISPAA YA IRINGA

Gari la zima moto likiwa limewahi kufika dakika chache tu baada ya moto huo kuwaka

Wakazi wa iringa wakionyesha ushirikiano wao



Majeruhi wakitolewa ndani

Binti huyu aliyekua amelala moto huo ukiwaka na tayari kawaishwa hospitalini


Umati wa wanairinga wakishuhudia ajali hiyo

Kikosi cha zimamoto kazini



MOTO unaosadikika kuwa chanzo chake ni Hitilafu (short) ya  umeme umeteketeza nyumba iliyopo maeneo ya Uhindini ambayo ni mali ya Bw.Mohamed Hazan. Tukio hilo limetoke leo majira ya saa 12:27 mchana kwa saa za afrika mashariki.
Hitilafu ya umeme ilisababisha moto kwenye godoro na baadae kuunguza paa la nyumba  hiyo.

Hata hivyo kikosi cha jeshi la Zima moto kiliwahi kufika eneo la tukio na kuokoa mali nyingi zilizokuwamo na majeruhi katika nyumba ya mfanya biashara huyo.


Katika tukio hilo watu wawili wamejeruhiwa na hakuna aliyekutwa na mauti kutokana na ajali hiyo.

Monday, 6 October 2014

HAYA NDIO MAMBO 7 MUHIMU YAKUFANYA ILI UWE NA AFYA BORA




exercise

Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuwa na afya bora katika mwaka huu wa 2011.Lakini kabla sijaendelea mbele sana,naomba niweke wazi kwamba afya bora haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake bali pia fikra chanya(positive attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba siku zote unakuwa na mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na watu wenye mawazo chanya.
1.Kunywa Maji kwa wingi- Bila shaka unakumbuka msemo “Maji ni Uhai”.Hiyo ni kweli kabisa.Maji ni uhai sio tu kwa mazingira yetu na dunia kwa ujumla bali pia kwa afya au miili yetu.Maji ni kitu muhimu sana kwa afya zetu.Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini.Maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.
Kiasi cha maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama vile unyevu(humidity) wa mahali ulipo,shughuli zinazohusisha mwili anazozifanya mtu na pia uzito wa mwili.Pamoja na hayo,kwa wastani miili yetu inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za maji.Vyakula tunavyokula huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili yetu.Kwa hiyo tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi 8-9 za maji kwa siku.
Njia rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya kutosha ni katika kuangalia mkojo. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi(colorless) au kuwa wa njano kidoogo.Kinyume cha hapo ni ishara kwamba hauna maji ya kutosha mwilini.Njia nyingine kutambua ni pamoja na kukaukwa na midomo(lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu cha mkojo.
Pata Usingizi wa Kutosha: Unakumbuka tulipokuwa wadogo wazazi wetu walisisitiza sana kwamba twende tukalale mapema ili tukue? Bila shaka walikuwa wanajua kwamba usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Ukiachilia mbali faida za usingizi kwa ajili ya afya za akili/ubongo wetu,usingizi au mapumziko ya kutosha ni muhimu kwa miili.Afya njema huenda sambamba na mapumziko.Ni wakati wa kuupa mwili nafasi ya kujijenga,kujiongezea nguvu na muhimu zaidi kuhakikisha kwamba tunakuwa na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo cha kuzeeka mapema.
Fanya Mazoezi- Hili linaweza kupita bila maelezo ya ziada.Mazoezi ni muhimu sana kwa afya bora. Fanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki.Jipatie muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Kama inawezekana nenda Gym.Badala ya kupanda lifti pale kazini kwako au mitaani,tumia ngazi za kawaida.Egesha gari lako mbali kidogo na unapokwenda ili upate nafasi ya kutembea nk. Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi hayatakiwi kuwa adhabu.
Faida za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali,kupunguza unene(bila shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa ya maradhi mengine)
Kula Matunda Kwa Wingi-Matunda ni chanzo kizuri sana cha madini na vitamins ambazo miili yetu inahitaji sana kwa ajili ya afya bora. Unajua kwamba machungwa,kwa mfano, yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C unavyobugia kila leo? Aina mbalimbali za matunda ambayo yana virutubishi vingi zaidi kiafya ni Parachichi(Avocado),apple,matikiti maji(cantaloupe),Zabibu(Grapefruit),Kiwi,Guava,mapapai,machungwa, strawberries nk.
Kula mboga za majani- Kama ilivyo kwa matunda,mboga za majani(vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Wataalamu wa afya wanashauri kwamba tule aina 5 mpaka 9 za mboga za majani na matunda.Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani na matunda.
Punguza Kula Vyakula vya Makopo- Kutokana na jinsi dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa muda wa kupika.Matokeo yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye makopo ambavyo ndivyo vimejaa katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya makopo huwa na ingredients ambazo hazifai kwa afya zetu.Kwa mfano,vingi miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo. Unaposhindwa kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia ambavyo havina sukari au chumvi.
Jipende- Kama nilivyodokeza hapo mwanzo,afya bora huenda sambamba na afya ya akili/ubongo.Njia mojawapo ya kupata afya hiyo ni pamoja na kujipenda.Pengine unajiuliza,kuna mtu ambaye hajipendi? Ukweli ni kwamba pengine ni kweli kwamba hakuna mtu ambaye hajipendi.Tofauti inakuja pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni kinyume kabisa na mapenzi ya mwili.
Mfano,uvutaji sigara,unywaji pombe kupindukia,kutojisafisha mwili wako kwa mfano kuoga,kupiga mswaki na pia kupumzika nk.Hizo zote ni tabia ambazo zinaweza kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako.Kama unaupenda utautumia vibaya au kuuharibu?