Agness Masogange Aingizwa Mkenge na Mnigeria na Kuikana Nchi Yake
Stori: Sifael Paul na Imelda Mtema
Habari ya mjini kwenye ulimwengu wa
mastaa Bongo ni taarifa kuwa video queen maarufu, Agness Gerald
‘Masogange’ amepatiwa passport (pasipoti) ya kuishi nchini Afrika Kusini
‘Sauzi’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara raia wa Nigeria.
MWANAUME KAMWINGIZA MKENGE?
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, ishu
hiyo ambayo imekuja miezi kadhaa baada ya ule msala wa Masogange wa
madawa ya kulevya ‘unga’ inadaiwa ‘imeinjiniwa’ na mwanaume huyo ambaye
haijajulikana kama naye amechukua uraia wa Sauzi au la.
KWA NINI MKENGE?
Ilisemekana kwamba ni mkenge kwa sababu
ili Masogange apate pasipoti hiyo, ilibidi aikane nchi yake ya kuzaliwa
ya Tanzania. Sheria za uraia wa Bongo kwa sasa zinakataza mtu kuwa na
uraia wa nchi mbili.
KIKAZI ZAIDI!
Awali, miezi kadhaa iliyopita ilielezwa
kuwa Masogange alitimka Sauzi kwa mwanaume huyo ambaye anadaiwa kufanya
naye ‘kazi’ (haikutajwa aina ya kazi) nchini humo.
Miezi kadhaa iliyopita Masogange
alionyesha kuukataa kabisa Utanzania, baada ya kuandika kwenye ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa kuanzia sasa hataitwa tena
Agness, bali umma umtambue kama Thando, jina lenye asili ya watu wa
taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika.
Pia Masogange alitupia mtandaoni picha
ya hati yake ya kusafiria ya Sauzi akidai kwamba maskani yake kwa sasa
ni kwenye Jiji la Johannesburg nchini humo.Kitendo hicho kinamfanya
Masogange ambaye ana asili ya Mkoa wa Mbeya, kuingia nchini kwa viza
kama wageni wa mataifa mengine wanavyofanya, wakipewa muda walioomba wa
kukaa au kufanya shughuli nyingine yoyote.
Kana kwamba haitoshi, endapo msichana
huyo atakumbwa na kosa lolote la kisheria akiwa nchini, anaweza
kufukuzwa na kutakiwa kutokuja tena, kama inavyotokea kwa wageni wengine
na hivyo kumnyima fursa ya kuwaona wajomba na mashangazi zake walio
Mahenge, Kondoa, Mkuranga na maeneo mengine Tanzania.
SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa sheria za Kibongo,
Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili (duo citizenship) hivyo Masogange
au Thando siyo Mtanzania tena.
MBALI NA MNIGERIA KUNA MSAUZI
Habari ziliendelea kuyeya kwamba mbali
na Mnigeria huku, Masogange anadaiwa kuwa na mwanaume mwingine, raia wa
Sauzi aitwaye Louis Dolnard ‘anayeminya’ naye nchini humo.
Kwenye Mtandao wa Instagram, mwanadada
huyo amekuwa akitupia picha za mahaba niue na mwanaume huyo huku
akidaiwa kumsifia jamaa huyo na kumpotezea aliyekuwa mchumba’ke, Evance
Komu.
MASOGANGE ANASEMA?
Akizungumza na gazeti hili, Masogange
anayeishi Mbezi-Beach jijini Dar, mara baada ya kukamilisha taratibu za
pasipoti hiyo kwenye ubalozi wa Afrika Kusini nchini, mrembo huyo
alikiri kukamilisha kila kitu hivyo kukwaa uraia wa nchi hiyo.
Kuhusu mwanaume huyo Mnigeria, Masogange
hakuwa tayari kuzungumzia lakini alipoulizwa juu ya yule Msauzi, video
queen huyo alikiri kumfahamu huku akigoma kufunguka zaidi.
TUMEFIKAJE HAPA?
Miezi kadhaa iliyopita, Masogange na
mwenzake Melissa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na
matirio ya kutengenezea madawa ya kulevya aina ya Crystal
Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8 ambapo katika hukumu ya kesi hiyo,
staa huyo alitakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za
Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela. Yeye alilipa faini hiyo akaachiwa
huru.