Siku
zote tunajua kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bwana Wilbroad Slaa ni mtu
mwongo, mnafiki na mzandiki ambaye moja ya sifa zake ni kupora na
kuoa mke wa mtu.
Lakini
sasa amekuwa kipofu aliyeona mwezi. Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Alhamisi, alidai kuwa amefanikiwa kunasa ratiba ya Mhe.
Rais Jakaya Kikwete kwenye safari yake ya China na kubwata mambo
mengi kuhusu ratiba hiyo.
Tatizo
langu mimi ni uongo wa Bwana Slaa kuwa ametumia mbinu zake kunasa
ratiba hiyo. Kwa nini nasema kuwa kauli hiyo ya Slaa ni uongo na
kuwarubuni wananchi.
Ukweli
ni kwamba ratiba ya Mhe. Rais mahali popote siyo siri. Ni jambo la
wazi kabisa ambalo linaafikiwa baada ya watu wengi kushirikisha
katika maandalizi ya ratiba hiyo.
Hivi
tunavyozungumza ratiba ya Mhe. Rais kwa ajili ya safari ya China
imechapishwa tayari kwenye kitabu. Na siyo ratiba tu, delegation
nzima ya nani Mhe. Rais anaambatana nao inajulikana, tena kwa majina
na nafasi zao, kwa sababu hili siyo jambo la siri.
Sasa
Slaa anavyowaeleza watu kuwa amefaniki kunasa undani wa ratiba ya
Rais Kikwete kule China anajaribu kumdanganya nani?
Huyu ni mtu ambaye anajaribu kuwa kiongozi wa Watanzania na
bado hana aibu wala aya kuwadanganya Watanznia hao hao kwa jambo
lililo wazi.
Tabia hiyo inathibitisha dharau ya Bwana Slaa kwa sisi
Watanzani. Ni mtu ambaye hafai kuwa kiongozi, kwa sababu kiongozi
hawezi kuwa mtu mwongo na mzandiki.
Na tumesikitishwa sana na
waandishi wa habari, kwani wamekubali kulishwa kila kitu na tena bila
kufikiria na kuuliza maswali wanaripoti katika vyombo vyao na
kushiriki kuudanganya umma wa watanzania.
No comments:
Post a Comment