Joyce Kasiki,Dodoma
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
Nape Nnauye amesema,kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (
Chadema ) kuzunguka Nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga katiba
inayopendekezwa,ni sawa na mtu kuzuia mafuriko kwa mikono.
Alisema
itakuwa vigumu kwa chama hicho kufanikiwa zoezi hilo kwani walitakiwa
kulishwishi kundi dogo la waliokuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
ili kuzuia theluthi mbili ya Zanzibar kupatikana huku akisema kuwa
wakati wao wanaendelea kuzuia mafuriko kwa mikono ,CCM kinajipanga
kuhakikisha kinashinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kura ya maoni ya
kupitishabkatiba inayopendekezwa.
Nape
alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakatinakizungumza wakati na
waandishi wa habari juu ya kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya chama
hicho (NEC) .
"Lakini
pia hawa Chadema wanasema watakwenda kupiga debe kujaribu kuzuia katiba
inayopendekezwa isipite ,lakini mimi salamu zangu kwao,kama walishindwa
kuzuia theluthi mbili bungeni ,mtaani hawataweza,wanaweza kuamua
kupoteza muda ,
"Na kwa kweli wanapoteza muda
sana kwa sababu katiba inayopendekezwa imebeba mambo mengi ya watanzania
ambao wapo tayari kuipitisha ,mimi ningedhani wangekuwa na akili
nyingi wangepambana kuzuia ile theluthi mbili ya kila upande
isipatikane Bungeni ,lakini waliposhindwa ile theluthi mbili,huku
mtaani tutawashinda asubuhi ." alisema Nape
Vile vile Nape alisema kikao cha Halmashauri Kuu kimeweka mikakati ya kuhakikisha chama hicho kinajitegemea kimapato.
"Halmashauri
kuu ilijadili sera ya chama ya kuwekeza kwa maana ya mikakati ya
kukifanya kijitegemee kimapato na siyonkutegemea ruzuku,
Alisema wakati umefika kwamchama hicho ambacho ni kikongwe nchini kujitegemea kimaato kwa kutengeneza sera ya uwekezaji .
Alisema
kuwa sera hiyo inalenga kuwa mwongozo wa kukifanya chama hiko kianze
kuzitumia rasilimali zake katika kuzalisha ili kiweze kujitegemea
kiuchumi.
“Kama inavyofahamika CCM ina
rasilimali nyingi wakiwemo wanachama wake,viwanja na majengo ambavyo kwa
pamoja vikitumika vizuri vitasaidia kukifanya chama kuondokana na
utegemezi wa ruzuku na badala yake kujitegemea”alisema Nnauye.
Vile
vile alisema NEC pia ilifanya uteuzi wa wagombea kwa nafasi za
Uenyekiti wa CCM katika Wilaya mbili ya Njombe na Misenyi pamoja na
wagombea Ujumbe kwa NEC katika Wilaya tatu ambazo ni Tandahimba,Mkuranga
na Njombe ambazo alisema nafasi zake zilikuwa wazi kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kufariki kwa viongozi waliokuwa wameshika nafasi
hizo.
Nape
aliwataja waluoteuliwa kugombea nafasi ya ujumbe wa NEC kuwa ni Lutavi
Suleman,Malela Chibwana na Nanyundu Salum kutoka wilaya ya Tandahimba na
Ally Msikamo,Khamis Zowage,Wakati Mtulia na Zawadi Kilapo kutoka wilaya
ya Mkuranga.
Wengine ni Christian Fwalo,George Mng'ong'o ,Oscher Msigwa na Justin Nusulupia kutkka wilaya ya Njombe.
Aidha
aliwataja wagombea wa nafasi ya wenyeviti wa wilaya ya Njombe kuwa ni
Edward Mgaya,Valence Kabelege na Betram Ng'imbudzi huku kwa wilaya ya
njombe wagombea kuwa ni Sostenes Kabandwa,Said Seruh na Erica Kiiza.
No comments:
Post a Comment