Friday, 17 October 2014

PATAMU HAPO::MAMA AMNG’ATA ULIMI ‘SERENGETI BOY’

Na Joseph Ngilisho, Arusha
HATARI! Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja aliyefahamika kama Mama Abuu amefanya tukio la ajabu baada ya kumng’ata na kumkata ulimi kijana Paulo Simon mwenye umri wa miaka 18, kufuatia ‘Serengeti Boy’ huyo kukataa kufanya naye mapenzi katika eneo la Tindigani, Kimandolu mjini Arusha hivi karibuni.
Kijana Paulo Simon aliyekatwa ulimi na mwanamke mmoja anayefahamika kama Mama Abuu.
Akisimulia kwa kuandika kwenye karatasi, Simon ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini hapa, alisema alikuwa akiuza baa katika eneo hilo wakati mwanamke huyo alipotokea na kukaa kaunta na kuanza kunywa pombe kama wateja wengine.
Alisema ilipofika saa 6:30 usiku wateja wengine wote waliondoka na kubakia mama huyo pekee, kitu kilichomfanya naye afunge baa. Lakini alipomaliza kufanya hivyo mama huyo alimfuata na kumweleza kuwa alihitaji kufanya naye mapenzi.
Kijana Paulo Simon(majeruhi) akiandika maelezo kwa Polisi kwa njia ya maandishi.
“Sikuwa na mazoea naye, nilipokataa kufanya naye mapenzi, alinisogelea na kunishika sehemu zangu za siri na kuanza kuzivuta, nilipopiga kelele akanishika kichwa na kunilazimisha ‘kunidendesha’, akafanikiwa kuingiza mdomo wake kwangu na kunikata ulimi wangu, akaondoka nao na kwenda kuutema karibu na mlango wa bar,” alisema Simon ambaye wahudumu wa hospitali hiyo wamelazimika kumwekea ndoo ili awe anatemea damu kutokana na kujaa mdomoni.
Alisema baada ya kukatwa ulimi ambao sasa unamletea maumivu makali, alifanikiwa kufika nyumbani kwake kabla ya tajiri yake kumchukua na kumpeleka hospitalini ambako amelazwa.
Jeshi la Polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni huku uchunguzi ukiwa unaendelea. Hali ya majeruhi inaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment