Friday, 15 August 2014

Apokonywa dhahabu kwa kuvua shati lake

 15 Agosti, 2014 

Mekhissi-Benabbad anawapungua watu mikono akiwa na shati lake mdomoni
Mwanariadha wa Ufaransa, Mahiedine Mekhissi-Benabbad amepokonywa medali yake ya dhahabu, aliyotarajiwa kuipata baada ya kushinda mbio za mita 3,000 za kuruka viunzi, katika mashindano ya riadha barani Ulaya.
Kilichomkuta mwanariadha huyu kilitokana na hatua yake ya kuvua shati lake alipokuwa anaelekea kushinda mbio hizo.
Mekhissi-Benabbad alivua shati lake na kuliweka kinywani pindi tu alipovuka msitari na kuibuka mshindi katika mbio hizo.
Awali, alionekene kupewa kadi ya manjani kama onyo na mmoja wa maafisa wa mashindano hayo ila hatimaye alipokonywa ushindi wake.
Mekhissi-Benabbad baada ya kutoa shati lake na kujifunika bendera ya ufaransa
"Mahiedine Mekhissi-Benabbad anawafanya watu kumchukia bure. Hapa alikuw ametengeza historia kwa kushinda medali hiyo lakini mara tu akavua shati na kuanza kulizungusha shati lile, na kujisababisia yaliyomkuba, '' alisema shabiki mmoja.
Timu ya uhispania ilionekana kuteta baada ya Murella kuvuka msitari na kuvua shati lake.
Mekhissi-Benabbad, 29, aliyeshinda medali ya fedha, siku za nyuma amewahi kusababisha utata baada ya kupigana na mwanariadha mwenza wakiwa wanakimbia mwaka 2011.