Mahakama imeafiki marufuku ya Suarez.
15 Agosti, 2014
Mahakama ya rufaa ya michezo imeafiki marufuku ya miezi miine aliyopewa mshambulizi wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez.
Hata hivyo Suarez amepata afueni kwani sasa ataruhusiwa kushiriki mazoezi na timu yake ya BarcelonaShirikisho la soka duniani FIFA ilimpata na hatia Suarez kwa kumn'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipokuwa ikikabiliana na Italia katika kombe la dunia huko Brazil.
Mshambulizi huyo wa Uruguay ataendelea kutumikia marufuku ya mechi za kimataifa .