Saturday, 16 August 2014

JE,TANZANIA ITAPATA KATIBA MPYA 2014?

Tanzania na katiba kulikoni?

Rais wa Tanzania , Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania , Jakaya Kikwete

Tanzania inaweza kutumbukia katika mpasuko wa kisiasa kufutia mzozo uliozuka kwenye bunge maalumu la katiba mjini Dodoma baada ya baadhi ya washiriki wa upinzani kujitoa.
Umoja wa katiba ya wananchi – UKAWA umegoma kuingia na kushiriki katika bunge la katiba hadi pale watakapofikia maridhiano ya nini cha kujadiliwa ndani ya bunge hilo.
Viongozi wa ukawa wamefanya mkutano na waandishi wa habari jumanne na kutishia kuitisha maandamano ya nchi nzima kama rais Jakaya Kikwete asipoingilia na kusitisha vikao hivyo.
serikali ya Tanzania Alhamisi imesema rais hana mamlaka ya kuingilia mchakato wa katiba kwa sasa. Lakini baadhi ya wapinzani waliogoma kuingia kwenye bunge hilo wameanza kugawanyika baada ya mbunge wa maswa magharibi John Shibuda , na Saidi Arfi mbunge wa mpanda kushiriki kwenye vikao hivyo wakidai kuwa wanatetea wananchi wao.
Wachambuzi wanaona hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, huenda katiba hiyo haitatumika kama malumbano hayatamalizika haraka iwezekanavyo.