Friday 12 September 2014

Aamrishwa kukoma kusambaza HIV

Jaji nchini Marekani amemuamrisha mwanamume mmoja mwathiriwa wa virusi vya HIV kukoma kusambaza virusi hivyo na badala yake kupata matibabu.
Inaarifiwa mwanamume huyo amewaambukiza watu 8 virusi kwa kukusudia katika kipindi cha miaka minne
Mwanamume huyo, aliyetambuliwa tu kwa herufi...'AO' katika stakabadhi zake, ametakiwa na mahakama kupata ushauri nasaha ili aweze kuwakinga wapenzi wake katika siku za usoni.
Maafisa wanasisitiza kwamba sio lengo lao kuufanya uhusiano wa kimapeni kuwa uhalifu bali wanataka zaidi kulinda umma.
Mwanamume huyo huenda akatozwa faini au kufungwa jela ikiwa hatafuata sheria kama alivyotakiwa.
Takriban watu 50,000 nchini Marekani huambukizwa virusi vya HIV kila mwaka , kulingana na shirika la kupambana na maambukizi (CDC).
Asilimia 16% ya watu milioni 1.1 wanaishi na virusi vya HIV bila ya kujua kwamba wameambukizwa.
Mwanamume huyo, alipatikana na virusi vya HIV mwaka 2008 na kuanza kusambaza kwa watu wengine na hadi sasa watu 8 wamethiriwa baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Alisambaza virusi hivyo licha ya kupokea ushauri nasaha ikiwemo kutumia kinga kila wakati anapojihusisha na tendo la ndoa.

No comments:

Post a Comment