........................................................................................................
MBUNGE wa jimbo wa jimbo la
Kalenga Godfrey Mgimwa ajipongeza kutumia kiasi cha zaidi ya Tsh
milioni 68 kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa ahadi zilizotolewa
na mbunge aliyefariki Dr Wiliam Mgimwa kwa asilimia 90 kwa muda
wa miezi mitatu pekee .
Akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Mangalali baada ya kukamilisha ahadi ya bati 100 kwa ajili ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lukwambe , mbunge
Mgimwa alisema kuwa alianza kutekeleza ahadi hizo hata kabla ya
kuapishwa bungeni na hadi sasa bado asilimia 10 pekee ya
utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge aliyefariki dunia mwanzoni
mwa mwaka huu marehemu Dr Mgimwa ambae alikuwa ni babake mzazi.
" Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu
kwani ahadi zilizokuwa zimetolewa na mbunge aliyefariki dunia
marehemu Dr wiliam Mgimwa zilikuwa ni asilimia 100 na hadi
mnanichangua kuwa mbunge ahadi hizo zilikuwa bado kutekelezwa na
ndio sababu ya mimi katika kampeni kutoahidi ahadi mpya zaidi ya
kuzipokea zile zilizoachwa na baba ambazo kimsingi nilizipokea
.......ila kwa sasa ahadi hizo nimetekeleza kwa asilimia 90 bado
asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani nitakuwa nimezimaliza kikubwa
naomba mzidi kuniombea uzima" alisema mbunge Mgimwa.
Alisema kuwa hakuweza kuahidi ahadi
mpya wakati wa kampeni hizo za uchaguzi mdogo jimboni humo kutokana
na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo zilikuwa zimetolewa na mbunge
aliyepita na zilikuwa bado kutekelezwa na muda wa utekelezaji
ulikuwa bado hivyo aliamua kuzichukua zote kama zilivyo na kuanza
kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine .
Mbunge Mgimwa alisema kuwa ahadi hizo
zinazotekelezwa ni zile ahadi binafsi ambazo mbunge aliyepita
alikuwa amezitoa ila zipo ahadi mbali mbali ambazo zimo katika ilani ya
CCM ambazo pia zimeendelea kutekelezwa kwa nguvu kubwa .
Hata
hivyo alisema kuwa ahadi ambazo zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo
zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja na elimu ,afya na uchangiaji wa
vikundi vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa vikundi hivyo pia katika
sekta ya michezo na huduma nyingine za kijamii kama upelekaji wa
umeme katika maeneo ya kata ya Mgama na Magulilwa zoezi hilo
linaendelea ambayo ahadi hiyo ya umeme ipo katika ilani ya CCM
pamoja na zile za huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi
kata ya Maboga na kata ya Lumuli wa maji unatekelezwa .
Pia alisema kuwa bado anautamani
ubunge wa jimbo hilo la Kalenga kwa mwaka 2015 -2020 hivyo kamwe
hatawaangusha wana Kalenga kwa kipindi hiki cha miaka miwili
alichopewa hadi 2010.
" Ndugu zangu hii nafasi ya ubunge
mimi nimeipata mwishoni ila sikutaka kuwaangusha nilitaka
kuwaonyesha utendaji wangu na kamwe sitakuwa mbali na ninyi wananchi
wangu nitakuwa bega kwa bega kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata
maendeleo na linakuwa ni jimbo la mfano katika maendeleo kule
bungeni kutokana na umri wangu wabunge wananiita bwana mdogo ila
kiutendaji kweli ni bwana mkubwa kwani kati ya wabunge zaidi ya 300
bungeni mimi ni mmoja kati ya wabunge tuliochanguliwa kuingia katika
kamati ya bunge ya bajeti ya serikali " alisema mbunge Mgimwa .
Awali katibu wa mbunge huyo Martine
Simangwa aliwaonya wana CCM ambao wameendelea kujipitisha katika
jimbo hilo na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wa
jimbo la Kalenga ambao kwa sasa wameshikamana na wapo tayari kuona
maendeleo na sio kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010.
" wapo baadhi ya wana CCM bila haya
wameendelea kujipitisha kwa wananchi na kuponda utendaji huu mzuri wa
mbunge Godfrey Mgimwa ....sasa wananchi nawaombeni sana
msidanganyike na watu hao kwa sasa mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na
kuwapa pesa chukueni ila msikubali kugawanywa kwa misingi ya pesa
kubalini kuungana katika misingi ya kimaendeleo"
Kwa upande wao wananchi hao walieleza
kufurahishwa na utendaji mzuri wa mbunge wao Mgimwa na kuwa kamwe
hawatakubali kudanganyika na kuwa wamejipanga kumchukulia fomu
mwakani ili kuwaongoza vipindi vingine viwili zaidi baada ya kuona
utendaji wake mzuri.
MWISHO
|
No comments:
Post a Comment