SIKU chache baada ya msanii mkongwe wa filamu Bongo, Lucy Komba kuolewa, msanii mwenzake, Wastara Juma ameibuka na kumpa somo la ndoa huku akimtaka kuwa mvumilivu na msiri katika maisha hayo mapya.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu na usiri mkubwa hivyo Lucy anatakiwa kuzingatia hayo kwani ndiyo siri ya kudumu kwenye ndoa lakini akiyakosa hayo atashindwa kuilinda ndoa yake kwani ndiyo sababu kubwa ya ndoa za mastaa kuvunjika.
“Nimefurahi sana Lucy kuolewa, namuombea Mungu amsaidie adumu kwenye ndoa mpaka kifo kitakapowatenganisha kama mimi nilivyotenganishwa na Sajuki lakini awe msiri, mvumilivu na mwenye hekima,” alisema Wastara.
Lucy alifunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake wa siku nyingi ambaye ni raia wa Denmark anayejulikana kwa jina la Janus ambapo baada ya hapo atakaa nchini kwa mwezi mmoja kwa ajili ya maandalizi kisha waelekee Denmark kwa mumewe.
No comments:
Post a Comment