WATU WATATU WANUSURIKA KUFA KWA AJALI DAR
Watu wawili
akiwemo raia wa China na dereva ambaye ni mtanzania wamenusurika kufa
katika ajali iliyotokea maeneo ya Millennium Tower, Kijitonyama jijini
Dar es Salaam ikihusisha gari ndogo aina ya Opa.
Mashuhuda wa
ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la zimamoto lililokuwa
linatokea njia ya Mikocheni kuingia barabara kubwa.
“Gari la fire
lilikuwa kasi sana huku likipiga king’ora, kwa hiyo kujihami dereva
mwenye Opa akajikuta ameingia mtaroni, tunashukuru hakuna aliyeumia,’’
alisema Robert.
Aidha mtu
mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo ni Abdukarim ambaye alikuwa
ndani ya mtaro huo akisafisha. Kamera ya GPL ilishuhudia askari wa
usalama barabarani akiwa eneo la tukio huku break down likianza kuitoa
gari hiyo mtaroni.
No comments:
Post a Comment