Askofu mkuu mstaafu wa kanisa la
Anglikan Tanzania Donald Mtetemela akizungumza na wadau wa mfuko wa "Mama
Bahati foundation" katika uzinduzi wa tawi la taasisi hiyo ya
kifedha mjini Mafinga katika wilaya ya Mufindi mkaoni Iringa.
Akinamama wadau wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," Wakiwa katika sherehe ya uzinduzi.
Pendo Donald Mtetemela akiwa katika uzinduzi wa tawi la Mafinga, tawi lililolenga kusogeza huduma ya mikopo kwa akinamama walio nje ya mji wa Iringa.
Pendo Donald Mtetemela (Kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," katika uzinduzi wa tawi la Mafinga.
Kalistus Lugenge, afisa mikopo wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akishuhudia uzinduzi huo kama ni sehemu ya kuongeza wigo wa huduma katika kuwafikia akinamama wengi zaidi walio wajasiriamali.
Elick Makamba mmoja wa maafisa katika mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akisikiliza jambo kwa umakini katika uzinduzi wa taasisi hiyo ya kifedha.
Askofu mkuu mstaafu Donald Mtetemela akiteta jambo na Evarista Kalalu - mkuu wa Wilaya ya Mufindi katika sherehe ya uzinduzi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation,".
Kulia ni mmoja wa marafiki wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akizungumza jambo katika siku hiyo ya uzinduzi mjini Mafinga.
Japhet Makau- Mkurugenzi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akizungumza lengo la kufungua tawi la mfuko huo mjini Mafinga.
ASKOFU mkuu
mstaafu Donald Mtetemela wa kanisa la Anglikan Tanzania, ambaye pia ni
mjumbe
wa bunge la katiba mpya, amewataka watanzania kuwa makini katika
kujadili suala
la nani atakaye kalia kiti cha urais awamu ya tano.
Askofu Mtetemela
ameyasema hayo- katika uzinduzi wa taasisi ya kifedha ya Mama Bahati
foundation, katika tawi la mafinga- Mufindi mkoani Iringa, tawi
lililoanzishwa
kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi waishio maeneo ya nje ya mji.
Mtetemela amesema
suala la watanzania kutazama umri wa rais ajaye– kama ni Kijana au mzee
si
jambo la muhimu bali ni kuchagua kiongozi atakayekuwa muadilifu mwenye
nia
thabiti ya kuwainua wananchi wake na Taifa kwa ujumla na ambaye atakuwa
ni
mnyoofu wa tabia, mwenye kutambua kuwa amebeba maisha ya watu.
Aidha amesema rais
wa awamu ya tano awe ni Yule anayetambua wajibu wake, mwenye dhamira ya
kulisogeza mbele Taifa kiuchumi na kuwa suala la umri lisiwe kipaumbele,
kwakuwa watanzania wanaweza kuchagua kijana au wazee ambaye
atalisababishia
hasara Taifa.
Akitolea mfano
wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.. Mtetemela licha ya kuwa
kiongozi
huyo alianza kazi ya kuliongoza taifa akiwa kijana hadi mtu mzima,
lakini busara zake zinaishi na zinahitajika
mpaka sasa katika kuliendeleza Taifa, na kuwa jambo la umri si
kipaumbele
sahihi cha kumpata kiongozi bora.
Akizungumzia
suala la tuhuma dhidi yake.. juu ya kuegemea upande wa siasa, Askofu
Mtetemela
amesema yeye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali anamsimamo
dhidi
ya mambo muhimu ambayo ni dira sahihi kwa Taifa, na kuwa kamwe hawezi
kuwa na
itikadi za kisiasa kutokana na ukweli kuwa waumini wake waliomtuma
wanatokana
na vyama mbalimbali.
Mtetemela
amesema pia yeye kama kiongozi hawezi kukwepa lawama kwa watu, na kamwe
hawezi
kukasirika anaposikia anazungumziwa iwe nikwa mazuri au mabaya
hatatakasilika,
na kuwa kuna umuhimu watanzania kuchagua kiongozi anayefanana kwa tabia
na
mwenendo kama baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
“Kwanza kiongozi
ninaamini kuwa tuhuma hupewa yoyote, na ukituhumiwa huwezi ukakasirika
ovyo
ovyo tu,!! Kupata hizo tuhuma si jambo geni kwangu, lakini pili
ningependa
nikanushe kuwa mimi siyo mwanachama wa chama chochote, iwe CCM, CHADEMA
wala
NCCR -maana kama ni kiongozi wa kidini waumini wangu wanatoka katika
vyama
mbalimbali- siwezi nikageuka nikawa wa chama kimoja, hiyo ndiyo kanuni
yangu
mimi,” Alisema Askofu Mtetemela.
Aidha amesema
hata kama tuhuma hizo za kuwa anafungamana na vyama vya siasa zinamfikia
yeye
hatua hiyo inatokana na msimamo wake kwani yeye anaunga mkono kitu
ambacho kipo sahihi, na hajali kimesemwa na
nani hata kama mtu asiyependana naye bali nini kimesemwa.
“Kwa mfano mimi
nilikemea bungeni nikasema siyo sawa mtu kuita bunge ni Intarahamwe,
nilikemea
kwa sababu sisi siyo wauaji, sikujali nani amesema, maana Intarahamwe
walifanya
mauaji kule Rwanda, sasa kama kuna watu wananipa tuhuma kwa sababu
wanataka niwe
upande fulani mimi siwezi kwani ninatoka kundi la 201katika kikundi cha
wajumbe
wanaowakirisha mashirika ya dini,”
Hata hivyo
Mtetemela alisema kamwe hawezi kutoka katika bunge hilo eti kwa sababu
kuna watu
Fulani wametoka, kwa madai kuwa yeye anao wajibu ambao amepewa na wale
waliomtuma
na mheshimiwa rais akamteua na kutoka kwake mpaka bunge linapokwisha
kisheria.
MWISHO
No comments:
Post a Comment