Mwanamitindo
Rio Paul (kulia) akiwa na rafiki zake muda mfupi baada ya uzinduzi wa
msimu wa pili wa Coke studio Africa, Hyatt Hotel, jijini Dar es Salaam.
Wanamuziki Vanessa Mdee, Jo Makini na Shaa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye 'red Carpet wakati wa uzinduzi huo.
Kutoka kushoto ni Joh Makini, Shaa, Bukuku (Mc wa shughuli hiyo), Maurice (bland meneja wa Coca-cola) na Vanessa Mdee.
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, jana usiku
ilizindua msimu wa pili wa onyesho la runinga lijulikanalo kama ‘Coke
Studio Africa’ ambalo linatarajiwa konyeshwa kila Jumatatu na kituo cha
Shirika la Utangazaji cha TBC.
Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo
uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt jijijini Dar es Salaam,
Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema, ni furaha
na fahari kwa watanzania na waafrika kwa ujumla kwa kukutana pamoja na
kuonyesha uwezo wa vipaji vyao hivyo, ambapo watu watapata kuona na
kujifunza vipaji na radha nzuri kutoka kwa wasanii 24 wa bara la Afrika.
“Muziki ni lugha isiyo na mipaka na njia muhimu ya kuonyesha hisia
na furaha, tungependa kusambaza furaha Barani Afrika kupitia muziki kwa
kushirikiana na wasanii,” alisema Njowoka.
Alisema, ujumbe wa msimu wa mwaka huu ni ‘Ushirikiano wa Afrika,
muziki wa afrika’, ambapo pia mbali na wasanii nyota pia wameweza
kushirikisha bendi, watayarishaji muziki na madj bora wa bara la Afrika.
Njowoka aliwataja wasanii hao kwa mwaka huu na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na Flavor Nabania,
Omawumi, Waje, Burna Boy, Chidima, Olamide, Iyanya, Seyi Shay,Yemi
Alade na Phyno (wote kutoka Nigeria), wengine ni Fena Gitu, Rabbit,
Victoria Kimani na Jay A (Wote kutoka Kenya), Navio, Jacie Chandiru na
Lilian Mbabazi (Kutoka Uganda), John Makini, Shaa, Diamond na Vanessa
Mdee (Kutoka Tanzania). Wengine ni Neyma, Jose Valdemiro na Marllen
(Msumbiji) huku watayarishaji wa muziki ni Silvastone (Ghana), Chopstix
na Afrologic (Nigeria), Kevin Provoke,Kagwe Mugai na Owuor Arunga
(Kenya) na wengieo.
Hata hivyo, mbali na kuonyeshwa kila Jumatatu kupitia runinga ya
TBC, mashabiki wanaweza kufuatilia pia kupitia tovuti ya Coke studio
ambayo ni www.cokestudioafrica.com.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali wakiwemo
wanamitindo, wabunifu, mamiss, wasanii wa filamu, muziki, vichekesho.
Mwisho
No comments:
Post a Comment