Nahodha wa
timu ya soka ya Liverpool ya England Steven Gerrard amesema amekuwa
anazionea wivu timu za Chelsea na Manchester United zikishindana katika
mashindano ya kombe la klabu bingwa barani ulaya.
Majogoo hao wa
Anflid watashuka dimbani siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza tangu mwaka
2009,kucheza na timu ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.'Tumekuwa tukisia tamaa na kuhisi wivu kwa kiasi kikubwa kwamba hatutashiriki kinyang'anyiro hicho,'' alisema Gerrard ambaye alishinda taji la michuano hiyo mwaka 2005
Nimekuwa nikitamani sana kuwepo. Kila mtu anazubiri kwa hamu kusikia muziki,'' alisema Gerard.
Chelsea wameshinda kombe hilo huku Manchester United wakimaliza katika nafasi ya pili tangu Liverpool kushiriki michuano hiyo miaka tano iliyopita. ''
No comments:
Post a Comment