Babu Tale: Fujo Kwenye Show ya Diamond Ujerumani ilipangwa Itokee Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale, anaamini kuwa fujo kwenye show ya msanii wake huyo jijini Stuttgart nchini Ujerumani ilipangwa itokee. “Sisi tumefanya kazi na promoter wa Nigeria, wao wenyewe kwanza ile advertize wakati wanamfuata Diamond hotelini hawakuwa wanaongea vizuri,” Tale ameiambia Bongo5. “Mmoja ni Mnaigeria mmoja sijui ni Msenegali.Ilikuwa imepangwa tu itokee, sometime vitu vingine vinapangwa tu ili vitokee, yaani kwa sababu, sio tumepanga itokee, imepangwa itokee, vitu vingine vinatokea for a reason,” ameongeza. Kama isingekuwa polisi wa Ujerumani leo tungekuwa tunaongea habari nyingine kwakuwa Diamond Platnumz aliponea chupuchupu kushambuliwa na mashabiki wenye hasira jijini Stuttgart nchini humo baada ya kuingia ukumbini saa 10 Alfajiri wakati mashabiki hao walikuwa wakimsubiri tangaa saa 4 usiku. Show hiyo ilikuwa ifanyike usiku wa kuamkia Jumapili. Katika tukio hilo lililoandikwa na vyombo vya habari vya nchini Ujerumani, promota wa show hiyo ambaye ni Mnaijeria alikimbia eneo la tukio na DJ wa show kupewa kipondo cha paka mwizi. Story kutoka Ujerumani inasema: Majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya mashabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show. Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi kwa Euro 25 kama kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo Diamond alipopelekwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event. Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake. Kilichowakera zaid mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hospitalini kwa sasa. Moja wa Djs hao alipoteza Laptop yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali. Mashabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani mashabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao. Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashtaka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara. Kupitia Instagram Diamond alidai kusikitishwa na tukio hilo. Kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kwa wingi kutusupport vijana wao, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi….
No comments:
Post a Comment