Yaani kwa kweli mambo ya hii dunia ni ya
ajabu na siku zote umdhaniae ndie kumbe sie kwa kweli, kuna rafiki
yangu ambaye kwa kweli si kama tuna urafiki sana lakini ni rafiki maana
tunaheshimiana nae sana na familia zetu zinafahamiana kwa kuwa tumejuana
kibiashara na si mambo mengine.
Mme ndiye ambae ninafanya nae kazi
ingawa mkewe namfahamu kwa kuwa ni sehemu pia ya msimamizi wa biashara
za huyo mwanaume. Jana nilikua na appointment na rafiki yangu ambae ni
daktari na ana hospitali yake.
Sasa wakati hiyo jana naingia nikakutana
na huyo mdada ambae ni shemeji yangu, tuka salimiana nikamuuliza vipi
hospital akasema ameenda kumcheki rafiki yake basi nikampotezea.
Sasa kumbe yule rafiki yangu dokta
alituona nikiongea nae, nlipofika kuzungumza na dokta maana namjua tabia
zake si za kistaarabu maana ni mdhaifu sana kwa wanawake, katika story
akaniambia amemtoa mimba ya wiki3.
Jamani mimi nimempokea Yesu na
nilimueleza dokta swala alilofanya ingawa ni rafiki yangu, lakini kitu
kingine ni kwamba mume wa huyu dada yuko nje ya nchi tangu july 21 na
atarudi mwishoni mwa mwezi huu kama mambo yataenda sawa ila hii
inamaanisha mkewe si mwaminifu kwa ujauzito wa wiki3.
je, nina haja ya kumwambia awe makini na mke wake kwakua si mwaminifu?
By bomouwa
No comments:
Post a Comment