Ujerumani kuwapa Wakurd silaha
1 Septemba, 2014
Ujerumani inatarajia kulitumia
jeshi la Wakurd wa Iraq silaha ikiwemo bunduki na silaha zile zenye
mfumo unaoweza kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita.
Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula
Von der Leyen amesema silaha hizo zotaweza kuwatosheleza wanajeshi elfu
nne ifikapo mwishoni mwa Septemba.
Amesema uamuzi huo ni kutokana na maslahi ya nchi yake.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani imeelezwa kuwa ni ya nadra sana kwa nchi hiyo, kupeleka silaha kwenye eneo lenye mapigano.
Hata hivyo uamuzi huo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wana wasiwasi zitakapoishia silaha hizo.

No comments:
Post a Comment