Monday, 1 September 2014

Dully Sykes atoa ushauri muhimu kwa Diamond na Alikiba

Dully Sykes atoa ushauri muhimu kwa Diamond na Alikiba

 
Msanii wa longtime kwenye familia ya Bongo Flava ambaye hujiita muasisi wa muziki huo, Dully Sykes amewataka Diamond na Alikiba kuweka tofauti zao na kufanya kazi pamoja

Dully amedai kuwa Alikiba na Diamond wanatakiwa wafanye kazi waweke tofauti zao pembeni na waingize hela. “Hivi we unadhani itoke nyimbo ya Alikiba na Diamond si itakuwa hatari sana! Maana hiyo ngoma itakuwa gumzo na pia wata watawafurahisha mashabiki wao. Huo ndo ushauri kwa wadogo zangu,” amesema Dully.

Katika hatua nyingine Dully ameiambia Bongo5 sababu za kutofanya vizuri kwa nyimbo zake za sasa. “Unajua nyimbo yangu kama ile ya “Joka” haikufanya vizuri kwakuwa watu walihisi kama nimemdiss mtu ndo maana haikufanya vizuri. Kwa wimbo wa “Binti Spesho” nao ulishindwa kufanya vizuri hasa ilivyofungiwa video yake lakini sasa wimbo wa ,’Togola’ unafanya vizuri nadhani pia umetoka kipindi kizuri na pia video yake ipo tayari inatoka muda wowote kuanzia sasa.

Kuhusu kazi yake kama mtayarishaji wa muziki, Dully amedai kuwa anazidi kuifurahia.

“Tokea nimekuwa producer naenjoy sana maana napenda sana kazi ya kuwa producer sasa hivi kuliko hata kuimba. Na pia sasa nimeshafanya kazi kadhaa za wasanii wakubwa zinakuja kama ya Chidi Benz vile imeshatoka na kuna zingine zinakuja. Unajua sasa hivi studio yangu ina vyombo vipya vya kisasa na pia ntakuwa narekodi live yaani napiga vyombo vyote.”

No comments:

Post a Comment