Sunday, 7 September 2014

Ushauri Kwa Wapinzani wa Lowassa Ndani ya CCM


Nimekuwa nikiona wapinzani wa Lowassa ndani ya ccm wakihangaika kila njia wakijaribu kuangalia ni namna gani wanaweza kumshughulikia jembe hili la kaskazini linalo mtanguliza Mungu mbele wakati wote wa mambo yake.

Lakini leo nimeona walau niwape ushauri kidogo baada ya kuona kila mnapo jaribu mnaangukia pua ni kwamba Lowassa ni mtu anaye mcha Mungu tofauti na wapinzani wake ndani ya CCM wamekuwa mara nyingi wanatumia nguvu za kiza na fedha nyingi wakifiri watamuweza Lowassa, lakini cha kushangaza mzee Lowasa amekuwa akizidi kuchanja mbuga kila kukicha na nyota yake kuonekana iking'ara kila siku japo kafungukiwa.

Naomba niwadokezee siri kuwa mgeukieni Mungu achaneni na nguvu za giza na mazingaombwe ndio njia tu ya kuweza kupambana na Lowassa japo mpaka muda kama ni soka basi tunaweza kusema Lowasa anaongoza kwa bao 3 bila,

Mkizingatia ushauri wangu mtasonga mbele epukeni kwenda kuchanjwa chale mwili mzima mrudieni Muumba atawasaidia.

By kiloriti

No comments:

Post a Comment