Waziri
wa Uchukuzi, Dkt Haririson Mwakyembe akiwa na Kamanda wa Kikosi cha
Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, wakiangalia gari la Mwanza Coach
walipotembelea eneoe la ajali jana.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Philipo Kalangi kulia, akiwa na Dkt
Harrison Mwakyembe, wakiangalia gari dogo aina ya Nissan Terano
linalodaiwa kupata ajali baada ya kugongwa na basi la Mwanza Coach na
kutumbukia mtoni.
Dkt
Mwakyembe, Waziri Gaudensia Kabaka na Dkt Samson Winani (mwenye shati
la kitenge) wakimwangalia mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimjulia hali Mwandishi wa Habari
wa Raia Tanzania, Veronica Mwakyembe ambaye alikuwa amelezwa Musoma.
Mawaziri Dkt Harison Mwakyembe na Gaudensia Kabaka walifurahia jambo wakati wakimjulia hali Frorance Focus.
Meya
wa Manispaa ya Musoma, Kisurura akimpa pole Kenneth Chilemile mkazi wa
Nyegezi Mwanza, aliypata ajali akiwa katika gari dogo aina ya Nissan
Terano, ambapo baba yake Ibrahimu Mashida pamoja na dereva wake
walipoteza maisha.
Wahudumu wa afya wakisaidiana kusukuma kitanda cha mgonjwa wa ajali ya Mwanza Coach na J4 Express.
Mwandishi
wa Mwananchi, Florance Focus akiwa amelazwa katika Hopitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mara baada ya kupata majeraha kichwani na miguuni. Hata hivyo
amehamishiwa Bugando kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Mkuu
wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa
Manispaa ya Musoma, Ahmed Sawa na Meya wa Manispaa ya Musoma, Kisurura
wa kwanza kushoto wakimjulia hali Mwandishi wa Mwanacnhi Florance Focus
baada ya kupata ajali.
Mwandishi
wa Channel Ten, Augustine Mgendi akimwangalia Veronica Mwakyembe
aliyepata ajali akisafiri na basi la Mwanza Coach. Mwakyembe ambaye ni
mwandishi wa habari wa Raia Tanzania amehamishiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Bugando kutokana na kupata mvunjiko kwenye bega na majeraha ya
mguu wa kushoto.
Waombolezaji
wakiwa wamebeba majeneza ya miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya
mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express wakienda kuzika katika makaburi ya
Musoma
No comments:
Post a Comment