Moja
ya shamba la viazi vinavyo subiriwa kuvunwa mwezi huu, shamba la
marehemu, Gabriel Mwasyebule, mashamba amabayo pia ni moja ya sababu
ambazo wananchi wa lwangwa wanamtuhumu marehemu kuwa alikuwa
anawalimisha watu kiuchawi na kuiba mazao ya mashamba mengine kiuchawi
ili shamba lake liwe na mazao mengi na mazuri.
MATUKIO ya kujichukulia sheria mikononi bado
yanazidi kuyakumba baadhi ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio
hili kijana Gabriel Mwasyebule miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira
kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja marehemu aliyetambulika kwa jina la Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande (Lwangwa) Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kifuani.
Alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumapili majira ya saa tano asubuhi huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoaniMbeya
Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo uliitisha kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi ya mavuno ya viazi na kujipatia pesa zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake aliyoweka marumaru na Gipsam pia kumiliki pikipiki moja huku akitarajia baada ya mavuno mazuri ya mwaka huu kununua gari la kutembelea.
Chanzo: Jamiiforums
No comments:
Post a Comment