Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba
yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa
washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo
hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii
nchini (ESRF)
SERIKALI
ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama
moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030
katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya
milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya,
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy
amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya
agenda za maendeleo.
“tunatambua
haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata
katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake
lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,”
amesema Balozi Mushy.
Amesema
kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika
Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda
ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
Mkurugenzi
wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini
(ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali
za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini
zinazoendelea.
Balozi
Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi
hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa
Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la
kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo.
Amesema
kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu,
huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa
umaskini wa kipato.
Balozi
Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia
yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia,
utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema
kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya
kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya
Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
Mkurugenzi
wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza
kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki
mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
“Watanzania
na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu
zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo
yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za
mwafrika,”aliongeza.
Kwa
upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward
Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa
yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya
wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo
tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania
imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya
ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt
Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika
Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia
lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
Mhadhiri
wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano
akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu
maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza
kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya
ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni
wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt.
Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa
Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha
ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye
jamii
Amesema
kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha
kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za
kutimiza malengo ya milenia.
Mdau
akichangia mada yake.
Wadau
wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
Wadau
mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment