CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Wilaya ya Mbeya mjini, kimpe siku tatu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi kukanusha kauli yake kuhusu kuwashughulikia Chadema
wakifanya maandamano.
Viongozi hao wa Chadema wakiongozwa na
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu) wametoa kauli hiyo katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya
Peak kufuatia baadhi ya magazeti kumnukuu kuwa atakaye andamana atafanyiwa kitu
kibaya ambacho hataweza kusahau maishani mwake.
Akitoa ufafanuzi juu ya Mkutano huo,
Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbeya mjini, Christopher Mwamsiku, alisema Chama
kimelazimika kuitisha mkutano na vyombo vya habari ili kukemea kauli aliyoitoa
Kamanda wa Polisi na kunukuliwa na baadhi ya magazeti.
Alisema Kauli aliyoitoa Kamanda Msangi
dhidi ya Chadema kwamba atakayeandamana atafanyiwa kitu kibaya ambacho
hawatakuja kukisahau katika maisha yao haipaswi kufumbiwa mdomo.
Awali akitoa Tamko kwa niaba ya Chama,
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema kama
chama kinatoa siku tatu Kamanda Msangi awe ameomba radhi kwa matamshi yake
hayo.
Alisema endapo atashindwa kuomba radhi,
Chama kiko tayari kuanza kukabiuliana naye kwa namna yoyote ile kwa maana
wanaamini Msangi hana Jeshi, Siraha, Bunduki na mabomu ya kuweza kuwashinda
Chadema wakiamua kupambana naye.
Alisema hivi sasa Redbriged ya Chadema
imeshafanya sense ya Askari wanaoishi uraiani pamoja na kuzitambua nyumba
wanazoishi ili akishindwa kuomba radhi watawalazimisha kurudi kwenye kota za
polisi.
Alisema kufanya hivyo ni kuwanusuru
endapo viongozi wa Chadema watapatwa na tatizo lolote hawataweza kunusurika kwa
kile Chadema itakachoamua kukifanya dhidi ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya, Ahmed Msangi, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo alikataa vikali kwamba
hakuwahi kuitoa na hawezi kutoa kauli kama hiyo kutokana na wadhfa alionao.
Alisema hayo maneno na yeye pia
aliyasoma kwenye gazeti kama Chadema walivyosoma hivyo hatua ya kwanza
aliyoichukua ni kuwapigia simu wahusika wa gazeti akiwalalamikia kumlisha
maneno ambayo hakuyasema.
Alisema anachokumbuka ni kwamba
Mwandishi wa habari hizo amewahi kumuuliza kuhusu kuwepo kwa maandamano ya
Chadema kupinga Bunge la Katiba nayeye kumjibu kuwa maandamano yamekatazwa
kote nchini hivyo atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kauli hiyo inalengo la
kuligombanisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Chadema lakini yeye binafsi
naushirikiano wa karibu na viongozi wa Chademana na kuongeza kuwa yeye sio
kiongozi wa Mtu mmoja bali kila mwananchi aliyepo Mbeya bila kujali chama
anachotoka.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment