Tuesday, 9 September 2014

Breaking news:KATIBA YA ZAMANI KUTUMIKA 2015..

Screen Shot 2014-09-09 at 5.39.36 PM
Ni taarifa kutoka bungeni ambayo itasaidia kukata kiu ya waliokua wanaisubiria au wanasubiri kufahamu kuhusu katiba mpya ambayo imekua ikiundwa, kama itatumika kwenye uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Ripoti kutoka  Dodoma zinaamplfy kwamba katiba ya zamani ndio itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka kesho 2015 lakini itafanyiwa marekebisho ambayo ni
1. kumpa ruhusa mgombea binafsi kugombea,
2. kuwa na tume huru ya uchaguzi ya kusimamia uchaguzi,
3. mshindi wa Urais ashinde kwa zaidi ya asilimi 50,
 4. matokeo ya uchaguzi wa Urais yaweze kupingwa Mahakamani,
 5. kuwe na tume huru ya kusimamia uchaguzi.
‘Vyama vya siasa vinavyopenda kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha katika katiba ya Jamuhuri ya muungano ya mwaka 1977 vinaombwa kufanya hivyo mapema’ – John Cheyo
Haya yametokana na kikao kilichofanyika kati ya Rais Kikwete na kituo cha demokrasia Tanzania ambapo Mwenyekiti wa kituo hicho John Cheyo.

No comments:

Post a Comment