Bomu lililotengenezwa kienyeji kama
linavoonekana katika picha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni
kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya
kulitegua bomu hili.
Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa
mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini
chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo
umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa
kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa
kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka
vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila
kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
-------------------------
Jeshi
la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la
wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa
katika eneo
la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la
utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya
saa moja
jioni.
Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa
kienyeji nawatu
wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika
kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa
ajili
kufanya kazi zao za kila siku.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa
milipuko
kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana
limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la
polisi
ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa
kienyeji
askari polisi watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini
manispaa ya songea.
Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya
jitihada za
kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na
ulipuaji,
Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi
ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya
namana hii.
Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya
songea
kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari
watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,
walijeruhiwa
kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo
lilisadikiwa
kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani
Ruvuma.
Askari
hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika
doria
ambao ni WP Felista Abel,
PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na
mtandao
huu wa demasho kwa njia ya simu amesikitishwa
na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani
iliyopo
katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha
amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama
watahakikisha
wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.
No comments:
Post a Comment