Thursday, 9 October 2014

MAHABA NIUE::DIAMOND ATESEKA NA PENZI LA WEMA!

Stori: Richard Bukos
Imebumburuka kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ kumbe anateseka na penzi la mwandani wake, Beautiful Onyinye Wema Isaac Sepetu, Amani lina mkanda kamili.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ akwa ameshika gauni la mpenzi wake.
YATOKANAYO
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa, Diamond amekuwa akiumia na kuvumilia anapoitwa majina mabaya huku akisemekana hamuwezi Wema hivyo awaachie mapedeshee wenye ‘kisu’ kirefu.
“Hivi unajua kwa nini Diamond alimpa Wema zawadi ya Nissan Murano (gari)? Alijua asipofanya hivyo kuna mtu atafanya  na kweli ndivyo ilivyotokea kwa lile Gari BMW.“Nawahakikishieni kwa Chibu au Dangote (Diamond) alichezwa na machale,” kilidai chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao.
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI YA DIAMOND
Sasa ndani ya pati ya bethidei ya Diamond kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, kidume huyo alinaswa akiwa ameshikilia gauni la Wema kwa muda mrefu ili kuhakikisha haliburuzi chini kwa urefu.
Akimshikia gauni la mpenzi wake huku wakiingia ukumbini.
Wakati wa kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya BMW X6 alilopewa na menejimenti yake, ndipo kulipokuwa na sarakasi kubwa kati ya mastaa hao.
DIAMOND AHANGAIKA
Baada ya wageni waalikwa kutangaziwa kuwa kuna zawadi maalum ya jamaa huyo, watu waliombwa kutoka nje kuelekea eneo la maegesho ya magari (parking) ili kushuhudia makabidhiano hayo.
Hapo ndipo Diamond alipojikuta akihangaika zaidi na gauni refu la Wema akilishikilia na mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshika glasi ya ‘waini’ nyekundu.
Wakati wakitembea mdogomdogo kama maharusi, Diamond alijikuta akiwa kama mpambe wa bibi harusi kwa kumzunguka Wema mara kwa mara akilishikilia gauni hilo, shukurani ziende kwa mbunifu wake maana mtoto wa kike alitokelezea mashalaah!
Diamond akimuweka sawa mpenzi wake.
UPAJA WA WEMA NJE
Kuna wakati Diamond alilinyanyua gauni hilo na kusababisha ule upaja mweupe wa Wema kuwa nje huku midume ikiutolea udenda na wengine wakihisi jamaa huyo alifanya makusudi ‘kuwaringishia’.
“Ebwana Chibu mbona anamfunua Madam upaja unaonekana? Au anaturingishia ili tujue anakaa pazuri?” alisikika mmoja wa wanaume hao bila kufafanua kukaa pazuri alimaanisha nini.
WEMA ACHEKELEA, ATEMBEA POLEPOLE
Wakati Diamond akihangaika na gauni hilo, Wema alikuwa akichekelea kwa kuonesha uso wa tabasamu na kutembea polepole ili kumhenyesha staa huyo na kuthibisha kwamba kweli yeye ni Madam na kwamba Diamond anajua ‘kukea’.
Wema na Diamond wakifanya yao.
KIJASHO CHEMBAMBA CHAMTOKA DIAMOND
Hadi wanafika kwenye zawadi hiyo ya gari, kijasho chembamba kilimtoka Diamond ambaye alipokea ufunguo kwa mkono mmoja baada ya kuomba ashikiwe glasi ya ‘waini’ huku mkono mwingine ukiendelea kushikilia gauni hilo hadi alipomfungulia Wema mlango akaingia, naye akazunguka upande wa dereva.
Baada ya kulitesti gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 90, wawili hao walirejea ukumbini kwa staili ileile ya Diamond kuhangaishwa na gauni hilo hadi walipoketi meza kuu na kuendelea na ratiba.
NI ‘KAMZIZI’?
Kwa mujibu wa watu wapenda ‘ubuyu’ waliokuwemo ukumbini humo walisikika wakisema si bure, Diamond kuhangaika na Wema kiasi hicho hivyo huenda kawekewa ‘kamzizi’.
“Mimi nakwambia hata kama ni kumpenda kiasi gani lakini hii ni zaidi ya mahaba niue au kawekewa kamzizi, si bure kwa wanaume wa kizazi hiki kukea kiasi hiki,” alisikika mmoja wa wanawake waliokuwa wakimuonea wivu Wema na kumpa pole Diamond kwa kuhenya.

No comments:

Post a Comment