Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioachishwa kazi.
ASKARI wa
Kikosi cha Usalama Barabarani waliopiga picha ya mahaba wakibusiana huku
wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi na picha yao ikasambaa katika
mitandao mbalimbali ya kijamii wamefukuzwa kazi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe amethibitisha leo kwa waandishi wa habari mkoani humo kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment