Wednesday, 15 October 2014

IRINGA::MKE wa mtu sumu , kikongwe afanya mauaji ya kihistoria Iringa

 Picha namba 01 Wananchi  wakiwasikiliza  mke  wa mtuhumiwa wa mauaji Bi  Melea Mtwanga akiwa na mtoto  wake  Manet Mtalima ( kushoto)  wakati  wakizungumza na mwandishi  wetu (hayupo pichani) nje ya eneo la tukio.
Mke  wa mtuhumiwa wa mauaji Bi  Melea Mtwanga akiwa na mtoto  wake  Manet Mtalima.
 


  Picha namba 02  mtuhumiwa wa mauaji Gwalino Ganga akiwa na mkewe  Melea  Mtwanga.


Na  Francis Godwin, Iringa
 
MKE ama mume  wa  mtu  ni  sumu si neno jipya  katika vinywa  vya wengi  japo baadhi yetu tumekuwa  tukichukulia juu juu neno ila kwa wakazi wa kijiji  cha Mbigili kata ya Mazombe wilaya ya Kilolo wameamini kuwa lina ukweli ndani yake baada ya kikongwe wa miaka 70 kumtwanga risasi mbili kijana ambae alimtuhumu kuingilia ndoa yake kwa  kuvunja amri ya sita na mama watoto wake.
 
Mbali ya kijana huyo Thadei Mbugu(40)ambae ni marehemu  kudaiwa kujihusisha kimapenzi na mke wa kikongwe huyo   Gwerino bado inaelezwa  kuwa chanzo cha mauti  yake alijisababishia  kutokana na maneo ya dharau ambayo  alikuwa akiyatoa mbele ya  watu  waliokuwa  wakinywa  pombe katika klabu cha pombe za  kienyeji kilichopo nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wa mauwaji ambacho kinaendeshwa na  mke wa mtuhumiwa  huyo wa mauwaji .
 
Imedaiwa  kuwa awali  mtuhumiwa huyo wa mauwaji alikuwa akimsaka mgoni  ama  dowezi  wake  ambae  amekuwa akiivuruga  ndoa yake bila  mafanikio  japo alikuwa na taarifa  kuwa  vijana  watoto  kijijini hapo  ndio  wanajihusisha kimapenzi  na mke  wake  huyo.
 
Akizungumza na mwandishi  wa  habari hizi  aliyefika  eneo la  tukio mke  wa  Maneti Mtalimbo (24) ambae ni  mtoto  wa kambo mtuhumiwa wa mauwaji hayo  alisema  kuwa chanzo  cha mauwaji hayo ni mke  wa marehemu kumtuhumu mama  yake  kuwa huwa na tabia ya  kukopa fedha kwa marehemu hali  iliyopelekea mama  yake  huyo  kwenda kumwita baba yake (mtuhumiwa) na kumshitakia maneno  hayo.
 
Baada ya  kufikishiwa malalamiko hayo mzee mtuhumiwa wa mauwaji  alifika  ndani ya klabu hicho na kuanza  kumuuliza marehemu  juu ya mahusiano  yake na mke  wake ndipo marehemu  alipoanza  kutoa  lugha chafu  mbele ya watu  kwa mwenye mke  kuwa ni masikini hana  uwezo wa  kutunza  wake wake  wawili hivyo anasaidia  kulea.
 
Alisema  kuwa  kufuatia madai hayo na majibu ya marehemu  kikongwe  huyo mtuhumiwa wa mauwaji alimtaka marehemu  kuondoka na katika  eneo hilo na mke wake mtuhumiwa kwa madai  kuwa wamependana  waende  wakaishi  wote ila marehemu aligoma na  kuendelea  kutoa  lugha chafu.
 
“Baba  alimtaka aondoke na mama kwa  kuwa  wamependana ila marehemu  alisikika akisema  siondoki  utanifanya  nini wewe  mzee  na baada ya  hapo akaanza  kumtukama  baba matusi kuwa   wewe ni masikini umeuza  ng’ombe nab ado  unaishi katika  vibanda ….baada ya  hapo  mimi nilitoka  kwenda  kutafuta msaada  wa watu kuja  kuamua  ugomvi  huo kwa kumtoa marehemu huyo ghafla  nyuma  nilisikia mlio  wa  risasi na baada ya  kurudi nilikutana na marehemu  huyo akitoka  nje  huku akivuja damu baada ya  kupigwa  risasi begani kushoto “
 
Alisema  baada ya  hapo  alilazimika  kuingia ndani na  kumuuliza baba yake  kulikoni  ila  kabla ya  kumuuliza  hivyo  Mbugu akiwa amelala  nje bila msaada .
 
“ Kweli  nilitoka  mbio kwenda  kutafuta  msaada wa gari  kwa  Besti  ili  sikumkuta  ila wakati najiandaa  kurudi baba alikwenda kumuongeza  risasi nyingine ya  kifuani na kumuua kabisa “
 
Hata  hivyo  baada ya  kumuua kabisa  ndipo alianza  kumfukuza mama yake mzazi akitaka  kumpiga  risasi kabla ya  kumfukuza na kumpokonya bunduki  hiyo na  wananchi  kusogea na kumtia nguvuni.
 
Huku mke  wa  mtuhumiwa  huyo  wa mauwaji Bi  Melea Mtwanga  akidai  kuwa hajapata  kuwa na mahusiano  yeyote na marehemu  huyo  isipo  kuwa marehemu aliuwawa kwa ajili ya  lugha zake  chafu .
 
“Marehemu  alikuwa akinidai pesa za mahindi  debe  kumi na  wakati akinidai ghafla  mume  wangu  alitoke na  kuuliza kwanini unaongea na mke  wangu na kusema  sasa  leo nakumaliza ndipo alipompiga  rusasi huku akiwa amekaa katika  benji  akinywa pombe na  wenzake …..kweli  watu  walikimbia wote japo  mimi  sikuwa na mahusiano yoyote na marehemu zaidi ya kunidai pesa za mahindi “
 
Alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo na maehemu  wote  walikuwa  wanamiliki wake  wawili  kila mmoja na kuwa  hakuona  sababu ya kufanyiana unyama  huo.
 
Mmoja kati ya  wajane  wa marehemu  huyo  Bi Gloria  Ngailo  alisema  kuwa  wakati mauwaji  hayo yakitokea  alikuwa eneo la  tukio  pamoja na mke  mwenzake ila  yeye  kwa  wakati huo alikuwa ametoka  nje ya chumba hicho kabla ya  kusikia mlio  wa  risasi na kusogea kukuta mume  wake akivuja  damu.
 
“ Siwezi  kujua kama ni kweli  alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtuhumiwa  japo tunaishi  jirani na mtuhumiwa  huyo ila ni kazi ya  nguvu ndie anayejua siri  iliyopo juu ya  tukio hilo”
 
Baba  mzazi wa marehemu  huyo  Antony  Mbungu alisema  kuwa haamini kama  mtoto  wake amekufa  na  kuwa hata kama alikuwa akimtuhumu  kutembea na mke wake  hukumu yake  haikuwa ni kifo .
 
Kwa  upenda  wao  mashuhuda wa  tukio hilo  walisema  kuwa wakati  linatokea  tukio  hilo  walikuwa ndani ya  chumba  hicho na kati yao  walikuwepo  vijana  wawili ambao  walikuwa  wakituhumiwa  pamoja na marehemu  kujihusisha na mapenzi na mke wa mtuhumiwa ambao baada ya  kuona mwenzao kapigwa  risasi walikimbia porini pamoja na walevi wengine   eneo hilo.
 
Mwenyekiti  wa  serikali ya  kijiji   hicho Bw  Chesco Lukosi  alisema  kuwa tukio hilo  limeacha  fundisho kubwa  kijijini hapo na kuwa ni  tukio la kwanza  kutokea kwa mtu  kuuwawa  kinyama  kiasi hicho.
 
Pia  alisema  iwapo  marehemu  asingekuwa na lugha  chafu  yawezekana  mauti  yasingemkuta ila kwa kawaida  wahehe  huwa  hawapendi kutukanwa  mbele ya wake  zao .
 
Alisema mauwaji hayo hayana tofauti mauwaji ya  aliyekuwa  mkuu wa mkoa  wa Iringa marehemu  Dr Kreluu aliyeuwawa miaka 40  iliyopita na mkulima Said Mwamwindi ambae  alimuua kwa mkuu  wa mkoa wa kumpiga  risasi na mwili  wake  kuupeleka polisi mwenyewe kabla ya  kukamatwa na kuhukumiwa  kifo .
 
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi amethibitisha  kutokea kwa  tukio hilo lililotokea Oktoba 9 majira ya saa moja za na  kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na  jeshi la polisi huku akidai  kuwa  bunduki  hiyo aina ya shotgun alikuwa akiimiliki kihalali .

No comments:

Post a Comment