WATU wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani hapa kwa
tuhuma za kuchoma moto jengo la masijala ya Idara ya Ardhi Manispaa ya
Kigoma Ujiji na kuteketeza nyaraka mbalimbali.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Japhari Muhamed, alisema jengo hilo
liliungua juzi majira ya saa 4 usiku baada ya kuchomwa na watu ambao
hawakujulikana.
Alisema kuwa mbinu iliyotumika ni kuchoma ofisi kwa kutumia
mafuta ya petroli ambako moto huo uliteketeza ofisi yote na kusababisha
hasara kubwa.
“Hakuna kitu kilichosalia baada ya moto kuteketeza ofisi, vyote
viliungua zikiwemo hati na nyaraka mbalimbali,” alisema Kamanda Muhamed.
Alisema wanawashikilia watu wanne kuhusiana na tukio hilo ambao
ni Anna Fanuel (46), mhudumu wa ofisi, Makrina Paulo (49), karani,
Saimon Pius (37), mkazi wa Burega na Tumaini Esau (44), mkazi wa
Mwasenga.
Kamanda Muhamed, aliongeza kuwa uchunguzi wa kina dhidi ya tukio
hilo unaendelea
No comments:
Post a Comment