Lorraine
Clement akimshukuru Mungu, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA), akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano
ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20
bora.
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorraine kiwa na familia yake na mama yake (kulia).
Na Andrerw Chale
MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na
kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika
mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10
jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine
aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye
mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline
Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema
bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG,
Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Katika mapokezi hayo, Lorraine
alilakiwa pia na wazazi wake pamoja na mtendaji Mkuu wa Redline
Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau wengine walijitokeza
uwanjani hapo.
Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru
watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya
Tanzania.
Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo
ambalo kwa hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication
Ltd, ambapo mshiriki wake huitwa ‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu,
Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top
Models 2013.
Aidha, Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi
ya Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss
Ethiopia, Hiwot Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut.
Shindano hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa
pili likifanyika nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa
mwaka huu, ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani
40,000, pamoja na thamani za ndani.
No comments:
Post a Comment