Waandamanaji
Hong Kong
Serikali
ya eneo la Hong Kong imeitisha mazungumzo maalumu na viongozi wa
wanafunzi ambao wamekuwa wakiratibu maandamano yaliyodumu kwa wiki mbili
hadi sasa.
Mkutano
huo wa serikali ya eneo hilo na wanafunzi unatarajiwa kufanyika
leo.waandamanaji hao wanapinga utawala wa Beijing kuwachagulia mgombea
katika uchaguzi mkuu wa eneo hilo 2017.
Hata
hivyo wanafunzi hao wamesisitiza kuwa wataendelea na mgomo huo pamoja na
serikali hiyo kuhitaji mazungumzo na viongozi wao.
Waandamanaji
hao kwa sasa wamekuwa wakiendelea na maandamano huku baadhi ya huduma
mhimu na kazi zikidorola.BBC
No comments:
Post a Comment