Hali bado sio shwari kwa wenzetu Kenya,
jana taarifa kubwa iliyoripotiwa kwa siku nzima kutoka kwenye nchi hiyo
ni ishu ya kuvamiwa kwa Chuo Kikuu cha Garissa, ambacho kiko karibu na mpaka wa nchi ya Somalia.
Wavamizi hao walivamia jana katika Chuo hicho na kuua walinzi wawili na baadae kuendelea kuwashambulia wanafunzi.
Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka sasa
ni watu 147, askari na Vikosi vya Jeshi la nchi hiyo wameendelea
kuzunguka maeneo ya Chuo hicho.
Shambulio hili ni kubwa, linafananishwa na tukio la uvamizi wa Shopping Malls za Westgate, Nairobi September 2013 ambalo lilisababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa.
Mpaka sasa wavamizi waliouawa ni wanne na mmoja wao amekamatwa.
Zaidi ya wanafunzi 500 walifanikiwa kutoka salama katika eneo hilo la Chuo.
No comments:
Post a Comment