Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Mtu mzima ovyoo! Akina mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la Heshima Pesa Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi mjini hapa wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu na kumwaga ‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo.

Wake
za watu wanaofahamika kama mama Sabra mwenye kigauni kifupi cha
draftidrafti, mama Jenifa mwenye kimini cha njano na mama Athuman
wakijitoa ufahamu mbele ya mahrusi.
Kwa mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la
aibu ya aina yake lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa
ambapo wanawake hao walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya
jirani yao.
Wanawake hao waliofahamika kwa majina ya
watoto wao ni pamoja na mama Sabra aliyekuwa akibinuka, aliyevalia
kigauni kifupi cha draftidrafti.Mwingine alikuwa ni mama Jenifa
aliyekuwa ametupia kimini cha njano na mama Athuman ambao kwa pamoja
walikuwa na vikuku miguuni.
Mtu wetu huyo aliyekuwa ndani ya ukumbi huo
aliwashuhudia wanawake hao wakimwaga lazi mara baada ya MC kuita kundi
lao kwa ajili ya kutoa zawadi.
Kabla ya kutoa zawadi, wamama hao
walimfuata DJ na kumtaka kuwawekea wimbo wowote wa Taarab, wakawekewa
ambapo wakiwa na zawadi yao ya doti moja ya khanga, walipita mbele ya
maharusi kwa mbwembwe zote na baada ya kukabidhi zawadi hiyo ndipo balaa
lilipoanza.
Huku wakipeana nafasi na mara nyingine kulaliana, walikuwa
wakijibinua na kuonesha staili za chumbani huku ‘makufuli’ yakiwa nje,
jambo lililotibua harusi hiyo.
Ilifika hatua hadi baadhi ya wazazi wakawa
wanawaziba watoto wasione, jambo lililosababisha wazazi wa pande zote
mbili (wakwe) kununa pamoja na MC wa shughuli hiyo, MC Chuma ambaye
baada ya kuona wanawake hao wanazidi kuvua nguo aliwashtua:
“Ninyi mnaofanya hivyo mjue OFM (Oparesheni Fichua Maovu ya Global
Publishers) ipo humu ndani, sasa kesho au keshokutwa msitafute lawama.”
Pamoja na angalizo hilo la MC, ndiyo kwanza wanawake hao walipozidi kumwaga lazi ikawa ni laana tupu.
Baada ya pati kukamilika, mwanahabari wetu aliwafuata wanawake hao na kuwahoji kulikoni kumwaga radhi kiasi hicho? Msikie huyu:
“Kazi yetu ni kuchangamsha sherehe. Shughuli ilipooza lakini baada ya
sisi kuserebuka, ilibadilika, habari ndiyo hiyo,” alisema mama Sabra.
Baada ya pati kukamilika, mwanahabari wetu aliwafuata wanawake hao na kuwahoji kulikoni kumwaga radhi kiasi hicho? Msikie huyu:
No comments:
Post a Comment