MWANDISHI WA MAREKANI AKATWA KICHWA
Foley
akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu mwandishi
huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani nchini Iraq.
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Kikosi cha kiislam cha kijeshi chenye
msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari
mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley. auawe