Tofauti na mastaa wengine ambao huandika majina ya wapenzi wao kwenye miili yao kuonesha jinsi wanalivyo na mapenzi nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu wamekuwa tofauti, Ijumaa limegundua.
Mastaa hawa wameonyesha kuwa na mapenzi na wazazi wao ambapo mwandishi wetu amebaini Diamond ameandika jina la mama yake mkononi huku Wema akiandika jina la baba yake mkononi pia.
Wote wamefanya hivyo kwenye mikono yao ya
kushoto sambamba na uwepo wa tatoo nyingine ambapo Wema ameandika ‘Daddy
Sepetu’ na Diamond akaandika Sandra…’
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wao wamedai huenda penzi la mastaa
hao si la kudumu ndiyo maana wamekwepa kuandikana ili isije ikawa shida
pale watakapomwagana
No comments:
Post a Comment