Friday, 10 October 2014

MTOTO ALBINO::Huyu ndio mtoto ambae Polisi wa Kenya wamemuokoa akija kuuzwa Tanzania.



K1


Kenya Polisi
Ni pale ambapo unaweza kuvuta picha baba anajaribu kufanya mbinu za kumsafirisha mtoto wake kwenda nchi ya pili ili akamuuze kwa watu ambao ameshazungumza nao kabisa na wako tayari wanasubiria biashara ifanyike.
Yani hiki kisa kilichotokea Kenya kina uzito wake mpana tu sababu Baba mzazi na Baba wa kambo wote wamehusika kwa nyakati tofauti kufanya mbinu za kutaka kumsafirisha mtoto huyu ambae ni Albino ili aje Tanzania kuuzwa na viungo vyake vitumike kwa imani za kishirikina.
K3 
NTV wameripoti kwamba Polisi wa Kenya ndio walimuokoa huyu mtoto akiwa tayari ameshaingizwa Tarime Tanzania akiwa anasafirishwa kwa siri na baba yake wa kufikia (wa kambo) ambapo mama mzazi amesema baada ya kuolewa na mume wa pili baada ya kuachana na yule wa kwanza ambae ndio baba wa mtoto, amekutana na kitu kilekile kama alichotaka kufanya mume wa kwanza, mume wa pili pia anataka kumuuza huyu mtoto.
Mama wa mtoto anasema ‘ninachoshangaa ni kwamba baba yake mzazi alipotaka kumuuza huyu mtoto alikamatwa, tena baba yake wa pili amejaribu kuja kutaka kuiba tena huyu mtoto, ni giza ambalo nimeliona kwangu na kuhofia maisha ya mtoto na mpaka sasa tunamfungia ndani hawezi kutoka hata kwenda shule’
Kwenye sentensi nyingine mama wa mtoto huyu anasema ‘Wakati mwingine najiuliza kwa sababu baba yake mzazi wa kwanza alishikwa na Polisi lakini sijui hiyo kesi iliendeleaje na akaachiliwa, sasa ni kama wameona ni  kawaida hata kama wanakwenda kuripotiwa hakuna hatua yoyote inachukuliwa kuhusu huyu mtoto’

No comments:

Post a Comment